Mjumbe Baraza Kuu JUVICUF awachambua Seif, Lipumba


Sharifa Marira

TOFAUTI ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad imetajwa kuwa ni utendaji kazi wao, huku mmoja akitajwa mwenye kinyongo na mwingine mpenda umoja.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Vijana (JUVICUF) Khomein Rwihula alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na JAMBO LEO kuhusu mgogoro wa pande mbili uliopo katika chama hicho.

Rwihula ambaye pia aliwahi kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu uliopita, alisema Lipumba anaendelea kufanya kazi ya kukijenga chama, hana kinyongo na mwanachama yeyote tofauti na Maalim Seif ambaye hafanyi kazi wala hafiki ofisini.

“Profesa Lipumba ni kiongozi wa mfano, yeye anafanya kazi tu, amejitahidi kumuita ofisini Maalim Seif ili aje ampangie majukumu ya kazi za kukijenga chama kwa mujibu wa katiba, lakini hajatokea,kazi yake ni kushughulika na kufukuza watu huko Zanzibar,’’alisema Rwihula.

Alisema Maalim Seif anapaswa kumuelewa Lipumba kuwa ana dhamira ya dhati ya kukijenga chama kwa kuwa hajatangaza mapambano na mtu isipokuwa amewaita kufanya kazi lakini hawajatokea.

Akizungumzia suala la CUF ya Maalim Seif kutangaza kwenda mahakamani kutafuta haki, alisema wanasita kutekeleza  jambo hilo kwa kuwa wamejua watakwama kutokana na Lipumba kutambulika kisheria.

“Tunajua kuwa sasa wanahangaika hawajui la kufanya kwa sababu wakiwaza kwenda mahakamani wameshajua kuwa itakula kwao, kwani katiba waliyoiandika wenyewe itawamaliza.’’

Alisema kinachotakiwa kufanywa na Maalim Seif na wafuasi wake ni kukubali kukaa meza moja ya mazungumzo na Profesa Lipumba ili waendeleze majukumu ya chama kama ambavyo anafanya kwa kupita kufanya mikutano mikoani.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo