Mabaraza ya ardhi yapungukiwa watumishi


Peter Akaro

MABARAZA ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya nchini yanakabiliwa na upungufu wa watumishi, vitendea kazi na ufinyu wa bajeti na kusababisha utendaji kuwa mdogo.

Hayo yalibahinishwa jana Dar es Salaam na Kaimu Msajili wa Baraza hilo, Amina Ntibampemba akisema hiyo ni changamoto kubwa kwani wanahitaji watumishi 411, kulinganisha na 179 waliopo.

“Tuna upungufu wa wenyeviti, makarani na wapiga chapa… kuna baadhi ya wilaya wenyeviti wanahudumia mabaraza zaidi ya matatu au mawili, wengine mkoa mzima,” alisema na kuongeza:

“Hali hii inachelewesha kusikilizwa kwa mashauri yaliyofunguliwa na wananchi, kutopata nakala za hukumu na mienendo ya mashauri kwa wakati, hivyo wananchi wengi wanalazimika kufuata huduma mbali za utatuzi wa migogoro,” alisema.

Amina alisema pia wanakabiliwa na mazingira yasiyoridhisha kwa kukosa ofisi, maktaba kwa ajili ya rejea za sheria na ukosefu wa samani na vitendea kazi. 

“Hali hiyo inachangia kuchelewa kwa ukaguzi wa maeneo ya migogoro kutokana na ukosefu wa usafiri,” alisema.

Alisema ili kukabiliana na changamoto hizo, Serikali inatakiwa kuhakikisha mabaraza ya ardhi yanakuwa na ofisi stahiki, wenyeviti na kuyapatia   vitendea kazi na fedha za kutosha.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo