Bodaboda wakataa kuwa ATM za Polisi


Sharifa Marira

WAENDESHA bodaboda wa Mbezi, Dar es Salaam wamemwomba Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kuingilia kati suala la askari Polisi kuwawinda na kuwanyang’anya pikipiki bila makosa ya kueleweka.

Mwakilishi wa madereva hao ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini akihofia usalama wake kutokana na kufahamiana na askari wanaofanya vitendo hivyo, alisema wamechoka kutumiwa kama mashine za kutolea fedha (ATM) na polisi.

Alisema kumekuwa na migogoro kati yao na polisi kwa kipindi kirefu, jambo linalowafanya kuwaona kama maadui zao namba moja wa maendeleo, kwani wanawakamata bila kuwa na makosa na kuwabambikia kesi.

‘’Tukikutana na polisi tunawaona kama maadui zetu, wametufanya kama ATM zao unakuta mtu huna kosa lolote anakukamata, anakwambia umekatiza katikati ya barabara ambayo si yako, ukijaribu kujitetea unakuta anataka umpe fedha, hawajali kwamba hujafanya biashara,’’ alisema.

Alisema imefika hatua wanatamani kuachana na biashara hiyo ili kuepuka kero wanayokutana nayo kwa askari hao kwani hakuna faida wanayopata.

‘’Tumekuwa msaada mkubwa kwa polisi, lakini wao hawatujali, tunaweza kukutana na tukio tukapeleka taarifa kituoni ila wao wanatuchukulia kama vitega uchumi vyao, kama bodaboda kafanya kosa mkamate mwandikie faini umwache afanye shughuli zake lakini si kumfuatafuata na kumbambika kesi,’’ alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo