Chama cha Wapangaji kuandaa sera ya ardhi

Celina Mathew

Ndumey Mukama (katikati)
CHAMA cha Wapangaji nchini kimesema kwa sasa kiko kwenye mchakato wa kuandaa sera ya ardhi ambayo itambana mpangaji na mpangishaji ili kuondokana na changamoto wanazokutana nazo hususan upandishaji kodi.

Akizungumza na JAMBO LEO jana, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Ndumey Mukama, alisema kwa kiasi kikubwa kukosekana sera hizo kumekuwa kukisababisha watu hao kukosa pa kujitetea.

Alisema baada ya mchakato wa kutoa maoni unaoendelea sasa, kukamilika sera hiyo itapelekwa kwenye Baraza la Mawaziri ili ijadiliwe na kisha kupelekwa bungeni, ambako kwa mara ya kwanza itasomwa kwenye Bunge lijalo.

"Tutakuja na sera ambayo itamwezesha mpangaji au mpangishaji kupanga gharama anayoitaka kwa kuwa kwa sasa haipo hivyo tunashindwa kuwabana kwa mujibu wa kanuni na sheria ambapo kila mmoja ataifuata," alisema.

Aliongeza kuwa kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakikemea hatua ya wenye nyumba kupandisha kodi, lakini kutokana na kuwa hakuna sera ya nyumba wanafanya wanavyotaka jambo ambalo huleta kero kwa wahusika.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo