Trump ‘atumbua’ mabalozi wote wa Marekani duniani


Washington DC, Marekani

Donald Trump
MUDA mchache baada ya kuapishwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump amewafuta kazi mabalozi wote wa nchi hiyo duniani na wanaofanya kazi katika mashirika ya kimataifa.

Trump amesema balozi katika nchi yoyote duniani ambaye aliteuliwa na Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama anatakiwa kuacha kazi mara moja.

Taarifa yake ya mabadiliko ilisema juzi kuwa hakuna msamaha kwa yeyote kuongeza muda hata kwa mabalozi wenye watoto wadogo.

Kutokana na tamko hilo, zaidi ya mabalozi 80 wa Marekani walio nchi mbalimbali duniani walifutwa kazi kuanzia Januari 20, mchana siku ambayo Trump aliapishwa.

Ni kawaida kwa nafasi za kuteuliwa kisiasa, ambapo mabalozi hujiuzulu unapoingia utawala mpya, hususan kinapoingia chama kingine madarakani.

Inaelezwa kuwa hatua hiyo ya Trump inaweza kuvuruga uhusiano muhimu na nchi kama vile Ujerumani, Uingereza na Canada. Ambapo nchi hizo zinaweza kukaa bila mabalozi kwa miezi kadhaa kwa kuwa baada ya Trump kuteua mabalozi wapya, watalazimika kuidhinishwa na Bunge la Congress kabla ya kuanza kazi.

Pia, nchi kama China, India, Japan na Saudi Arabia nazo zinatazamiwa kukumbwa na mabadiliko hayo.

Uteuzi ambao umefanywa mpaka sasa ni wa Gavana wa South Carolina, Nikki Hayley ambaye anakuwa balozi kwenye Umoja wa Mataifa akichukua nafasi ya Samantha Power.

Mwanasheria wa Ufilisi, David Friedman ameteuliwa kuwa balozi Israel na Gavana wa Iowa, Terry Branstad ameteuliwa kuwa balozi China. 

Trump amekosolewa kwa kuacha nafasi nyingi wazi na hivyo kuvuruga shughuli za kawaida za Serikali ya Marekani.

Hayo yanajiri huku maandamano yakiripotiwa kote duniani dhidi ya kiongozi huyo. Imeripotiwa kuwa kumefanyika maandamano 637 katika maeneo mbalimbali ya Ulaya, Asia na Afrika kumpinga.



Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo