Dawati la Ulinzi kuanzishwa shuleni


Mwandishi Wetu, Morogoro

Sihaba Nkinga
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inakusudia kuanzisha dawati la ulinzi na usalama katika shule zote na kamati za ulinzi na usalama ngazi za kata na vijiji nchini kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Sihaba Nkinga, alisema hayo jana kwenye ufunguzi wa kikao cha Kamati  Kuu  ya   Baraza   la  Watoto  la  Taifa cha siku mbili mjini hapa.

Aidha, aliwataka wajumbe wa kikao hicho kujadili kwa kina ongezeko la vitendo vya ulawiti na ubakaji dhidi ya watoto na kuwasilisha mapendekezo yao wizarani.  

Aliongeza kuwa kutokana na kuzinduliwa kwa mpango mkakati wa kupambana na kuzuia ukatili dhidi   ya   wanawake   na   watoto   wa   miaka   mitano,   Serikali   itahakikisha   vitendo   vya   ukatili vinapunguzwa kwa asilimia 50 kupitia mpango kazi huo.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Caroline Augustino akizungumza na vyombo vya habari alisema Baraza hilo limefanya ziara mikoani kuandaa makala maalumu za uelimishaji jamii kwa njia ya redio na runinga, ili jamii ifahamu maana na aina za ukatili dhidi ya watoto.

Caroline  aliwataka   wasichana   wa   umri   mdogo   kuachana   na   tamaa zinazowafanya   kujiingiza   kwenye   matendo   mabaya   yanayosababisha   kukatisha   ndoto   zao ikiwamo kushindwa kuendelea na masomo kwenye ndoa za  utotoni na kutaka wazazi na walezi kutambua kuwa mtoto wa kike ana fursa sawa na wa kiume hasa vijijini.

Pia alizitaka jamii za wafugaji na baadhi za Kanda ya Ziwa kuacha tabia ya tohara mbili kwa watoto wa kiume na ukeketaji kwa watoto wa kike kwani inasababisha vifo na maumivu ambayo yana athari mbaya za kipindi kirefu.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo