Mbowe: Nitatoa yamoyoni nikifika Hai


Leonce Zimbandu

Freeman Mbowe
MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema atafunguka na kuzungumzia mambo yote yanayohusu deni linaloelezwa kuwa inadaiwa hoteli yake ya Aishi Machame atakapofika jimboni kwake Hai.

Mbowe ametoa kauli hiyo baada ya gazeti hili kumtaka azungumzie tuhuma zinazomkabili, baada ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Gellasius Byakanwa kudai amekwepa kulipa kodi ya huduma ya biashara kwa miaka mitano.

Alisema kwa kipindi hiki hawezi kuzungumzia sakata hilo hadi atakapowasili katika jimbo lake la Hai ili kujua ukweli wa tuhuma hizo ambazo zimetangazwa na Mkuu wa Wilaya.

“Siwezi kuzungumza chochote, kwani sifahamu kinachoendelea. Lakini nikifika jimboni nitafunguka na kubainisha ukweli wa tuhuma hizo,” alisema.

Jana gazeti hili ilichapisha habari kuwa baada ya sakata la Club Billicanas kuamiriwa kuhama katika jengo la Shirika la nyumba la Taifa (NHC) mwaka jana kutokana na kudaiwa deni la sh.bilioni 1.3 la pango.

Katika sakata hilo jipya la Hoteli ya Aishi Machame Mkuu wa wilaya Byakanwa alidai kuwa Hoteli hiyo iliandikiwa barua Januari 21, mwaka jana na kutakiwa kulipa kodi lakini barua hiyo haikujibiwa.

Mbali na barua hiyo kutojibiwa Byakanwa alidai kuwa Hoteli hiyo haijapeleka taarifa ya mauzo ya kila mwaka katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa miaka mitano kwani taarifa hiyo ingetumika kukadiria kodi.

Kutokana na madai hayo, Byakanwa aliamua kutoa siku 14 kwa Uongozi waHoteli hiyo kulipa kodi hiyo ya huduma ya biashara inayofikia sh. milioni 13.5, vinginevyo huduma hiyo itasitishwa.

Katika hatua nyingine Byakanwa amesitisha shughuli za kilimo katika shamba linalimilikiwa na Mbowe kwa madai kuwa lipo ndani ya chanzo cha maji yam to Weruweru.

Hivyo aliagiza Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya tathmini ya uharibifu wa mazingira katika eneo hilo uliofanywa na Mbunge wa Hai ili hatua zichukuliwe.

Pia Mkuu wa Wilaya ya Hai Byakanwa aliwataka maafisa Maliasili wa Wilaya kufanya tathmini ya miti iliyokatwa bila kibali na kuleta kiasi cha faini ndani ya siku 14 ili hatuya zifanyike.

“Huyu ni kiongozi wa kitaifa tena kioo cha jamii anapaswa kuwa mfano kwa wananchi anaowangoza, sfanyi hilo kwa kumwonea mtu hali nazingatia sheria,” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo