Wizara yasaidiwa samani na China


Leonce Zimbandu

Nape Nnauye
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante ole Gabriel amepokea msaada wa samani za ofisi zenye thamani ya Sh milioni 5.9 kutoa kampuni ya Jianexi Geo - Engineering Group ya China.

Samani hizo ni meza 11 na viti 11 kwa ajili ya kusaidia watendaji wa Wizara kufanya kazi katika mazingira bora na kuongeza ufanisi wa utekelezaji majukumu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea vifaa hivyo juzi, Profesa Gabriel alisema msaada huo umewafikia muda mwafaka ili kuimarisha uhusiano uliodumu miaka 50.

Alisema msaada huo ni moja ya uwajibikaji kwa jamii, hivyo wadau wengine wa sanaa wanaombwa kuiga mfano huo wa kampuni ya Geo – Engineering kutoa msaada.

“Samani hizo za ofisi zitafungwa katika ofisi zetu za Dodoma huku Wizara ikiendelea kujiandaa kuhamia,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jianexi Geo - Engineering Group, Chen Xianghua alisema wametoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji wao kwa jamii.

“Tunashukuru msaada huo kupokewa, hivyo tutaendelea kutoa misaada ili kuendeleza na kukuza ushirikiano wa kijamii,” alisema.

Ofisa Utamaduni kwenye Ubalozi wa China nchini, Gao Wei alisema Kampuni hiyo imetoa msaada huo kupitia ubalozi wao wa china baada ya kupokea maombi mbalimbali.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo