Anne Kilango amshukuru Mungu kuteuliwa mbunge


Emeresiana Athanas

Anne Kilango
ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango, amemshukuru Rais John Magufuli kwa kumteua kuwa Mbunge huku akisema Mungu ni mwaminifu.

Aidha kutokana na uteuzi huo, ameahidi kufanyakazi kwa kushirikiana na wabunge wenzake na kurejesha heshima ya chama hasa katika kipindi hiki cha kuleta maendeleo.

Kauli hiyo inakuja siku moja baada ya Rais kumteua Kilango kuwa mbunge wa viti maalumu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kilango alisema Mungu ni mwema na kumshukuru Rais kwa kuonesha imani na uaminifu kwake.

"Namshukuru Rais kwa kuonesha imani yake kwangu, naamini nitaenda kufanya kazi ipasavyo," alisema.

Alisisitiza kuwa kazi aliyoteuliwa ameifanya kwa muda wa miaka 15 kupitia Jimbo la Same, kwa jitihada kubwa na kuahidi kuendeleza jitihada hizo kwa kushirikiana na wabunge wenzake.

Alisema atafanyakazi kwa bidii zote katika kuhakikisha anakipa heshima chama chake.

April 11 mwaka jana Rais alitengua nafasi ya Kilango ya Mkuu Wa Mkoa wa Shinyanga na Katibu Tawala wa Mkoa, Abdul Dachi okufuatia mkoa huokutia taarifa zisizo sahihi kuwa hauna watumishi hewa.

Kutokana na taarifa hiyo, Rais alituma timu ya ukaguzi ambapo Aprili 10 mwaka Jana ilitoa taarifa ya kubaini kuwepo kwa watumishi hewa 45 mkoani humo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo