Kizimbani kwa kunajisi mwanafunzi


Moses Ng’wat, Rungwe

FARAJA Sweli (28) mkazi wa kijiji cha Ndaga, wilayani hapa amefikishwa mahakamani akituhumiwa kumnajisi mwanafunzi (jina limehifadhiwa) wa darasa la pili.

Akisoma mashitaka dhidi ya Sweli mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilaya ya Rungwe, Paul Ntumo jana, mwendesha mashitaka wa Polisi, John Asalile alidai kuwa, mtuhumiwa alitenda kosa hilo Januari mosi.

Alidai kuwa kabla ya kutenda uovu huo, alivamia nyumbani kwa wazazi wa mwanafunzi huyo waliokuwa wamelala usiku na kumnajisi na kumsababishia maumivu makali.

Akifafanua, mwendesha mashitaka huyo alidai pia kwamba mtuhumiwa akiwa na lengo la kufanya uovu huo alimchukua mwanafunzi huyo mbele ya dada yake wakiwa wamelala saa nane usiku huku akamtishia dada huyo.

Kutokana na shauri hilo, upande wa mashitaka uliwasilisha mashahidi watatu mahakamani hapo na kutoa ushahidi kabla ya hakimu kuiahirisha kesi hiyo hadi Februari 13.

Siku hiyo, Mahakama itaendelea kusikiliza mashahidi waliobaki wa upande wa mashitaka.



Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo