Upelelezi wakwamisha kesi ya Ndama


Grace Gurisha

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imeutaka upande wa Jamhuri kwenye kesi ya kutakatisha fedha haramu inayomkabili mfanyabiashara wa Dar es Salaam, Hussein Ndama (44) kuharakisha upelelezi.

Agizo hilo lilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo,Victoria Nongwa, baada ya Wakili wa Serikali Leonard Challo kumwambia kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Challo aliiambia Mahakama kuwa kesi ilikuja kutajwa, upelelezi haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine ya kuangalia kama utakuwa umekamilika.

Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Nongwa aliiahirisha kesi hiyo hadi Januari 24, itakapotajwa. Mshitakiwa amepelekwa rumande kwa sababu moja kati ya mashitaka yanayomkabili la kutakatisha fedha halina dhamana.

Ndama anadaiwa kuwa Februari 20, 2014 Dar es Salaam,  alighushi  nyaraka za kibali cha kusafirisha madini na sampuli zao kuonesha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited iliruhusiwa kusafirisha makasha manne ya dhahabu ya kilo 207 yenye thamani ya dola 8,280,000 kwenda Australia  kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo