JPM uso kwa uso na Guterres Addis Ababa


Hussein Ndubikile

Rais John Magufuli
RAIS John Magufuli ameanza kuhudhuria Mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari  na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa ilieleza kuwa jana asubuhi Rais Magufuli alihudhuria  mkutano ulioitishwa na Mwenyekiti wa umoja huo, Idriss Deby Itno na kwamba wakuu wa nchi za umoja huo watakutana na Katibu Mkuu Mpya wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres.

Malengo ya mkutano huo ni kubadilishana mawazo juu ya namna ya kuboresha uhusiano kati ya umoja huo na UN hususan katika kuimarisha masuala ya usalama.

Msigwa alisema kuwa mkutano huo utafuatiwa na mkutano maalumu wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika utakaongozwa na mwenyekiti wake.

Alisisitiza kuwa rais Magufuli alikula chakula cha mchana kilichoandaliwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika (AUC), Dk. Nkosazana Zuma lengo likiwa kutangaza rasmi jina la kituo kipya cha usalama na amani kilichopewa jina la Mwalimu Julius Nyerere kutokana na kutambua mchango wake katika kupigania amani na usalama wa Afrika.

Pia, alisema kituo hicho kipo ndani ya majengo  ya Makao Makuu ya AU mjini humo, huku akiongeza kuwa rais Magufuli alitoa hotuba fupi baada ya kukitangaza.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo