Wafungwa maisha jela mara mbili


Jemah Makamba

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imewahukumu kwenda jela maisha mara mbili na miaka mingine 30 Jackson Simon, Kalambo Matiku na Marwa Mwita wote wakazi wa Kipunguni, Dar es Salaam kwa ujambazi, kujeruhi na kunajisi watoto.

Hukumu hiyo ilisomwa jana mbele ya Hakimu Juma Hassan ambaye alisema katika ushahidi uliotolewa na shahidi wa kwanza ambaye ni mtoto wa mlalamikaji, ilidaiwa kuwa siku ya tukio Julai 27 mwaka juzi wakiwa nyumbani Kipunguni wamelala, saa nane usiku walishitushwa na kelele za baba yao akiomba msaada.

Baada ya hapo walisikia kitu kikimpiga baba yao na kushuhudia washitakiwa hao wakiingia chumbani mwao na kutokana na mwanga wa taa waliwatambua ndipo akasikia mmoja akisema: “Haiwezekani yule dereva bodaboda atudanganye, mbona hatuoni pesa?”

Kisha waliwatolea kisu watoto hao ambao mmoja alikuwa na miaka 12 na mwingine 15 na kuwalawiti kwa zamu.

Washitakiwa baada ya hapo walichukua televisheni, mabegi mawili ya shule na simu mbili na kuondoka, watoto walipoingia chumbani walimkuta baba yao amefungwa kamba.

Walikwenda kuamsha majirani ambao walikwenda kuripoti kituo cha Polisi cha jirani   na kesho yake kuhamia kituo cha Sitakishari na msako wa kuwatafuta ukaanza.

Kwa kuwa washitakiwa waliiba simu polisi walifanya utafiti kupitia kampuni moja ya simu na kugundua mmoja kati ya washitakiwa alikuwa akitumia simu hiyo na kumkamata baada ya kumtegea mtego.

Baba aliyefanyiwa tukio hilo alidai kupigwa nondo kichwani na kuchomwa kisu na kisha kufungwa kamba kabla washitakiwa hao hawajahamia kwenye chumba cha watoto.

Shahidi mwingine ambaye ni mtoto aliyelawitiwa ushahidi wake ulifanana na shahidi wa kwanza ambaye ni dada yake.

Daktari wa Hospitali ya Amana alifika mahakamani hapo na kuambatanisha fomu za uchunguzi (PF3) ambayo ilionesha watoto hao kunajisiwa na kulawitiowa na baba kujeruhiwa.

Washitakiwa walikutwa na kesi ya kujibu na katika utetezi wao, mshitakiwa wa tatu alikataa kujitetea na kunyamaza kimya huku wengine wakisema hawajahusika.

Hakimu alimuuliza mwendesha mashitaka, Grace Mwanga kama kuna kumbukumbu za nyuma za makosa ya washitakiwa akasema hakuna ila wanastahili adhabu kali ili kuwa fundisho kwao kutokana na kitendo walichofanya.

Hakimu aliwauliza kama wana cha kuimbia Mahakama kabla hajawapa adhabu, wa kwanza aliomba kuachwa, wa pili akisema atakata rufaa na mwingine akakaa kimya.

Hakimu alisema kutokana na makosa yao matatu waliyofanya, la kwanza ni jela miaka 30, la pili na la tatu jela maisha kila moja.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo