Lissu kusomewa maelezo ya awali leo


Grace Gurisha

Mahakamani
MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mhariri wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina, wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi leo wanatarajia kusomewa maelezo ya awali, baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.

Mbali na Lissu na Mkina, washitakiwa wengine ni Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.

Washtakiwa hao watasomewa maelezo hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Thomas Simba ambaye ndiye anayesikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Jana washtakiwa hao walitakiwa kusomewa maelezo hayo, lakini hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi leo kutokana na kwamba alikuwa na kesi nyingine za kusikiliza..

Alisema kesi hiyo itasikilizwa mapema kwa sababu anakesi zingine na kusikiliza.

Washtakiwa hao wanatetewa na Wakili Peter Kibatala. Awali, hakimu huyo alishangaa upande wa Jamhuri kushindwa kumkamata Lissu licha ya kwamba yeye alitoa hati ya kukamatwa kwa Mbunge huyo.

Hata hivyo, alimueleza Lissu kuwa aachane na mambo anayofanya kwa sababu yeye ni kioo cha jamii, kwa hiyo hastahili kufanya anayoyafanya na pia yeye ni mwanasheria na ajua sheria.

Ilidaiwa Januari 12 hadi 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, washtakiwa watatu, Jabir, Mkina na Lissu, kwa pamoja waliandika na kuchapisha taarifa? za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.

Wakati huohuo, Mahakama hiyo imeahirisha kesi nyingine ya uchohezi ‘Dikteta uchwara’ inayomkabili Lissu kwa sababu upande wa Jamhuri hawakuwa na mashahidi hadi Februari 14 mwaka huu kwa kusikilizwa.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo