RC Arusha kupanda kizimbani kesi ya Lema


Mery Kitosio, Arusha

Mrisho Gambo
MKUU wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, anatarajia kupanda kizimbani kutoa ushahidi katika kesi ya kusambaza ujumbe wa kuudhi kwa njia ya mtandao, inayomkabili mbunge wa Arusha Godbless Lema na mkewe Neema.

Wengine wanaotarajia kutoa ushahidi katika kesi hiyo ni mkuu wa upelelezi wa polisi mkoa wa Arusha, RCO George Katabazi, mkuu wa upelelezi wa wilaya (OC CID), Damas Masawe na kampuni ya simu ya Vodacom.

Lema (40) na Neema (33) wamepanda kizimbani leo katika Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha na kusomewa maelezo ya awali katika shauri la jinai namba 51 la mwaka 2016.

Mbunge huyo anashtakiwa kwa kosa la kumtumia ujumbe kwa njia ya mtandao kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo

Akisoma maelezo hayo mbele ya hakimu, John Baro wa mahakama hiyo, wakili wa Serikali Alice Mtenga alisema mshtakiwa Lema Agosti 20 mwaka 2016, alituma ujumbe kupitia simu yenye namba 0764170745 mali ya mkewe Neema Lema kwenda namba 07667575757 mali ya mkuu wa mkoa wa Arusha.

Mtenga alisema upelelzi wa kesi hiyo umekamilika na wanatarajia kuleta mashahidi watano na vielelezo viwili ambavyo ni simu ya mshtakiwa na karatasi yenye ujumbe wa mashtaka.

Wakili wa upande wa mshtakiwa wakiongozwa na John Malya baada ya kusikiliza maelezo hayo, alisema kuwa hati ya mashtaka imekosewa na kuitaka Mahakama iondoe shauri hilo mahakamani.

Hata hivyo, hakimu Baro aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 3, mwaka huu atakapotoa uamuzi au sikilizwaji wa kesi hiyo.

Wakati huo huo, kesi ya jinai namba 352 ya mwaka 2016 inayomkabili mbunge huyo imeunguruma leo mahakamani hapo.

Katika kesi hiyo Lema anashtakiwa kwa kosa la kuchochea maandamano ya kupinga udikteta maarufu kwa jina la Ukuta. Kesi hiyo ilikuwa kwa hakimu mfawidhi Agustino Rwezile wa Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha. Kwa sasa kesi hiyo inasikilizwa na hakimu Bernad Nganga baada ya hakimu Rwezile kuhama kikazi.

Mwanasheria wa Serikali, Alice Mtenga aiiambia Mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, ambapo alisoma maelezo ya awali kwa Mshitakiwa.

Hata hivyo, upande wa mstakiwa ukiongozwa na wakili John Mallya walidai kuwa kesi hiyo inayomkabili mshtakiwa ni yakikatiba kwani alilenga kutoa maoni yake kama mwananchi wa kawaida.

Alisema ibara ya 18 yakatiba ya jamhuri ya muungano Tanganyika ya mwaka 77 inatoa haki kwa mshitakiwa ama raia mwingine kutoa maoni yake.

Malya alisema kesi hiyo inapaswa kusikilizwa na mahakama ya katiba chini ya majaji watatu, jambo ambalo hakimu Nganga alisema atalitolea uamuzi mdogo Februari 8 mwaka huu.

Mbunge Lema alirudi magereza kutokana na kesi ya uchochezi dhidi ya rais magufuli ambayo bado haijampatia dhamana hadi sasa.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo