Wizara yatoa tahadhari ya ugonjwa wa mafua ya ndege


Mwandishi Wetu

SERIKALI imetoa tahadhari ya ugonjwa wa mafua ya ndege, ikitaka wananachi kuzingatia kanuni za afya za kuzuia ugonjwa huo.

Imetoa tahadhari hiyo kufuatia kubainika uwepo wa virusi vya mafua makali ya ndege katika nchi jirani ya Uganda.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Waziri wa Afya, Jinsia, wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ilisema kuwa hadi sasa ugonjwa wa mafua ya ndege haujaingia, lakini kuna haja ya kuchukua tahadhari.

Ummy alisema ugonjwa huo uliosababishwa na ndege pori, hauangalii mipaka, hivyo kunahitajika kuchukuliwa tahadharii madhubuti ili kuzuia usiingie nchini.

"Wananchi wanatakiwa kuzingatia kanuni za afya za kuzuia ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa mara moja wanapoona vifo vya ndege au kuku. Pia wanatakiwa kuripoti haraka kwenye vituo vya kutolea huduma za afya mara wanapoona dalili zozote za ugonjwa huu," alisema .

Hata hivyo alitaka wananchi kutojenga hofu kuhusu ugonjwa huo, kwani haujaingia nchini, badala yake wajitahidi kuudhibiti usiingie.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa maeneo yalioathirika kuwepo kwa ugonjwa huo ni yanayozunguka Ziwa Victoria na ziwa lenyewe, huku ikieleza kuwa umengundulika baada ya kuwepo kwa vifo vingi vya ndege pori katika eneo ya Lutembe beach, Masaka, Kachanga, Bukibanga na Bukakata ya nchini Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo vifo hivyo vimetokea kwa baadhi ya ndege wafugwao (kuku na bata), huku ikihisiwa kuwa ndege hao wamepata virusi vya ugonjwa huo kutoka kwa ndege pori wanaohama kutoka nchi za Ulaya.

"Vifo hivi vya ndege pori vilianza kuonekana tangu Januari 2, mwaka huu na vimeonekana kuendelea hadi sasa, wakati kwa hapa nchini hakuna vifo vya ndege vilivyoripotiwa hadi sasa," ilisema taarifa hiyo.

Hata hivyo, pamoja na ukweli kwamba hadi sasa hakuna binadamu yeyote aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo nchini Uganda, bado tunahitaji kuwa makini,” alisema
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo