Serikali yaunga mkono mgomo wa wavuvi


Aidan Mhando, Mwanza

SIKU chache baada ya wavuvi 2,000 wa Ziwa Victoria kutangaza mgomo kwa siku zisizojulikana kwa madai kuwa Serikali inawakandamiza kutokana na sheria mbovu ya uvuvi, Serikali imesema mgomo huo ni faida, kwani itatoa nafasi ya kukua kwa rasilimali zilizopo kwenye Ziwa hilo.

Kauli hiyo inakuja ikiwa tayari Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa kushirikina na Hifadhi ya Usimamizi wa Rasilimali za Ziwa Victoria, kukamata wavuvi haramu 14 na zana haramu za uvuvi ikiwamo nyavu 1,660.

Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa Mfawidhi wa Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Kanda ya Mwanza, Lameck Mongo alisema mgomo huo kwao ni faida, kwani utasaidia kuongezeka samaki ambao wamekuwa wakivuliwa kinyume na sheria.

“Serikali itahakikisha hatua stahiki zinachukuliwa kwa watakaoshiriki uvuvi kinyume na sheria za uvuvi zinavyotaka. Watu wanapaswa kutii sheria na kuacha kutafuta sababu zisizo na msingi. Hatuwezi kuacha watu watumie nyavu zisizoruhusiwa kuvua samaki,” alisema Mongo.

Mongo alisema watu waliotangaza mgomo huo ni kikundi cha wachache, kwani bado shughuli za uvuvi zinaendelea Ziwa Victoria kama kawaida na waendelee na mgomo huo tu kama wanataka.

Alisema sheria ya uvuvi ya mwaka 2003 kifungu cha 22, inatoa maelekezo ya uvuvi ikiwamo kuzuia kuvua kwa zana haramu na kanuni za sheria hiyo za mwaka 2005 kifungu cha 52, H, K zinakataza kuunganisha nyavu haramu.

Hivi Karibuni, Msemaji wa Chama cha Wavuvi Kanda ya Ziwa (TAFU), Sijaona James alisema wanataka na mazungumzo ili kupata majibu ya pamoja ikiwamo Serikali kufanya mabadiliko ya sheria ya uvuvi.

Serikali imekuwa ikiendesha operesheni dhidib ya uvuvi haramu, ikiwamo katika Ziwa Victoria.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo