Wajawazito washauriwa kuanza kliniki mapema


Suleiman Msuya

WAJAWAZITO wameshauriwa kuanza kliniki miezi mitatu baada ya kugundua kuwa wana mimba ili kuepusha magonjwa ambayo yanawakumba katika kipindi hicho.

Ushauri huo umetolewa na Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndungulile ambaye kitaaluma ni daktari wa kutibu binadamu wakati akizungumza na JAMBOLEO jana ambalo lilitaka kujua sababu zinazosababisha vifo vya wajawazito nchini.

Alisema pamoja na utafiti kuonesha kuwa asilimia 51 ya kina wajawazito ndio wanahudhuria kliniki bado kuna changamoto ya walio wengi kujifungulia majumbani.

Mbunge huyo alisema kitaalamu mjamzito anapaswa kuanza kliniki miezi mitatu baada ya kujigundua kuwa mjamzito.

Alisema iwapo wajawazito watazingatia taratibu za kiafya ni dhahiri madhara yanatokana na mimba yatakuwa yanapungua siku hadi siku.

Dk Ndugulile alisema utafiti unaonesha kuwa kati ya wanawake 100,000 ambao wanajifungua, 555 wanapoteza maisha nchini idadi ambayo ni kubwa na kuwa sababu ya vifo hivyo ikiwa ni kifafa cha mimba, shinikizo la damu, kutokwa na damu na maradhi tofauti.

Alisema asilimia 63 ya wajawazito ndio wameonekana kujifungulia hospitalini hiyo ikionesha kuwa asilimia 37 wanajifungulia katika mazingira yasiyo sahihi.

“Unajua mwanamke kupata mimba ni sifa ya ukamilifu wa afya yake na tambua kuwa mimba si ugonjwa hivyo kuumwa mjamzito si kipaumbele katika mimba,” alisema.

Alisema kinachohitajika ni wajawazito kufuata taratibu za uzazi kwa umakini ikiwa ni pamoja na kula vyakula ambavyo vina kinga mbalimbali.

Mbunge huyo alisema wajawazito wanapaswa kujiepusha na msongo wa mawazo, presha ambazo huwa zina matokeo ya kusababisha kifafa cha mimba.

Aidha, alisema hata changamoto za kimaisha zinasababisha magonjwa yasiyotarajiwa kwa wajawazito.

Akizungumzia wilaya ya Kigamboni, alisema kitakwimu hali ni nzuri tofauti na vijijini na kuwa sababu kubwa ni kuwepo vituo vya afya ambavyo vina kila huduma yakiwamo magari ya kubebea wagonjwa.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo