MoI yaridhia `kijana mrefu zaidi’ akatibiwe ughaibuni


Salha Mohamed

JOPO la madaktari wa Taasi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MoI), limeridhia kijana Baraka Mashauri (35) mwenye urefu wa futi 7 anayesumbuliwa na nyonga akatibiwe nje ya nchi.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Ustawi wa Jamii cha Moi, Jumaa Almas alisema madaktari hao waliokuwa wanafuatilia matibabu ya Mashauri walifikia hatua hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Wazee na Watoto.

“Tumeamua kumpeleka nje ya nchi baada ya kubaini kuwa gharama za matibabu yake kwa hapa nchini ni kubwa,” alisema na kuongeza kuwa alihitajika kuwekewa pandikizi (implant) kinachotakiwa kuagizwa nje ya nchi.

Almas alisema pamoja na kupunguza gharama za matibabu zinazogharamiwa na Serikali, kutibiwa nje kutawezesha kupatikana matibabu ya uhakika na uhakika wa pandikizi kuliko hapa nchini ambapo zingeagizwa tatu kutoka nje ya nchi ili kupata moja ya inayofaa.

“Ikumbukwe kwamba vifaa hivyo (pandikizi) vinatengenezwa kwa `oda’ maalum hivyo gharama ni za juu ikilinganishwa na kupelekwa nje ya nchi,”alisema.

Mashauri ni mgonjwa wa kwanza kupokelewa MoI akiwa na urefu ambao haujawahi kudhihirika kwa mwingine kabla na baada ya kufika hospitalini hapo mwishoni mwa Oktoba mwaka juzi, akitokea Majita B mkoani Mara, ili kutibiwa nyonga kwenye mguu wa kushoto.

Kwa mujibu wa Almas, mgonjwa huyo ameibua changamoto nyingi zinazotokana na urefu wake ikiwamo kushindwa kupata kitanda miongoni mwa vinavyotumika kwa wagonjwa wa upasuaji vyenye urefu wa futi sita.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo