Watanzania watakiwa kumuenzi Nyerere


Haji Kameta

Mwalimu Julius Nyerere
WATANZANIA wametakiwa kuishi kwa kuenzi falsafa za baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere ili kuifanya jamii kuwa mahala salama pa kuishi.

Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Kitengo cha Falsafa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk. Adolf Mihanjo ambaye alifafanua kuwa watu wanatakiwa kufanya tafakuri ya kina kuhusu dini kuepuka migogoro.

Alisema hayo katika mkutano wa amani ulioandaliwa na Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Watu wa Iran na kufanyika semina ya siku moja.

"Inatakiwa vijana wafundishwe kufikiri kwa kina ili kupata ufumbuzi wa fikra na katika hilo tutashirikiana na wenzetu wa Iran kwani wao wanauwezo mkubwa katika ukombozi wa fikra,"alisema.

Mwalimu wa Falsafa na dini, Evarist Magoti alisema yeye ni mwakilishi wa dini za jadi na amani. Alisema kuwa waumini wa dini za sasa wanatakiwa kujifunza kupitia dini za jadi kwa maana hizo zina historia kutokana na ukweli kuwa ndizo zilizopokea Ukristo na Uislamu.

"Tunatakiwa kuziangalia dini za jadi kwa sababu zina uzoefu wa kuishi na dini zote na kutunza amani kwa muda wote, hivyo ili tupate amani tunatakiwa kulinda tamaduni zetu," alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo