Wachimbaji 14 wafunikwa kifusi mgodini


Aidan Mhando, Geita

WACHIMBAJI wadogo 14 wa mgodi wa dhahabu wa RZ wa kata ya Nyarugusu mkoani hapa, akiwamo raia wa China, wamefunikwa na kifusi cha udongo kutokana na maporomoko kwenye moja ya mashimo walilokuwa wakichimba.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na baadhi ya wachimbaji wenzao zilieleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 9 alfajiri wakati wachimbaji hao wakiendelea na uchimbaji wa dhahabu.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali mstaafu, Ezekiel Kyunga ambaye alikuwa ziara ya kikazi mkoani humo, alisitisha ziara yake ili kutembelea eneo la tukio.

Kyunga aliagiza uokoaji uanze mara moja na kubainisha kuwa hadi anaondoka eneo la tukio, ulikuwa ukiendelea bila mafanikio kutokana na kutofikiwa kwa wachimbaji hao.

Tukio hilo lilitokea takribani miezi 14 tangu wachimbaji watano wa mgodi wa Nyangarata, Kahama mkoani Shinyanga, kuokolewa wakiwa hai baada ya kufunikwa na kifusi cha udongo ardhini kwa siku 41.

Wachimbaji hao waliokolewa Novemba 16 mwaka juzi, baada ya kufunikwa Oktoba 5 na kubainisha kuwa waliishi siku hizo zote kwa kula wadudu kama mende na mizizi huku wakitumia kofia kukinga maji yaliyokuwa yakitiririka kutoka juu na kunywa.

Watu walioshuhudia tukio hilo lililoacha kumbukumbu ya aina yake nchini, walisema ardhi ya juu ya machimbo hayo ilititia na kuporomoka kutokana na mvua iliyonyesha na kuwafunika. Katika jitihada za uokoaji, waliokolewa wachimbaji watano.  
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo