Wafanyabiashara Tanzania, Uturuki kuunda Baraza


Mary Mtuka

Godfrey Simbeye
TAASISI ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imeingia makubaliano ya kuanzisha Baraza la Kibiashara na Uturuki kwa lengo la kukuza biashara za hizo nchi mbili.

Makubaliano hayo yalifikiwa Dar es Salaam juzi kwenye kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, alisema Baraza hilo litaratibu juhudi za pamoja, kukusanya, kuunganisha, kuchambua, kuthamini na kueneza taarifa zinazohusu biashara na   ushirikiano kwenye uwekezaji.

Alisema Baraza litaanzisha na kukuza viwanda, kupitia ushirikiano wa teknolojia wa mashirika na taasisi za kiuchumi za Uturuki.

“Baraza litaandaa maonesho ya kibiashara na kuhamasisha wanachama wake kushiriki     na hatimae kuwezesha wajasiriamali wadogo na wa kati kuwapa ujuzi na maarifa,” alisema Simbeye.

Aliongeza kuwa kutakuwa na ukusanyaji wa takwimu na taarifa juu ya fursa za biashara na kusambaza taarifa kwa wanachama.

Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi alisema wafanyabiashara na Watanzania wote wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo kwa kuwa Uturuki ni mabingwa wa kilimo ambacho Watanzania wengi wanakitegemea.

Pia Mengi alimshukuru Rais John Magufuli kwa kumleta nchini Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki kwani kwa wafanyabiashara ni fursa ya pekee ya kufungua milango ya biashara zao.

Hata hivyo, alisema kwa kushirikiana na Baraza hilo litaunda kamati mbili, kila moja ikiwa  na wajumbe wake na taasisi za kiuchumi.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo