Miamala ya simu yapitisha Sh 13.07 trilioni


Peter Akaro

ZAIDI ya Sh 13.07 trioni zimepita katika mitandao ya simu katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tcra), imesema.

Kaimu Meneja wa Mawasiliano, Semu Mwakyanjara alisema jana kuwa kiasi hicho cha fedha kilipita kwenye mitandao hiyo kati ya miezi ya Novemba na Desemba.

“Mwishoni mwaka jana kwa mwezi Novemba na Desemba kwa wastani fedha zilizopita katika mitandao ya kampuni za simu Sh. trilioni 13.07,” alisema Mwakyanjara na kuongeza;

“Kwa mwezi Novemba ilikuwa ni Sh. trilioni 6.47 na Desemba Sh. trilioni 6.60.”

Katika hatua nyingine, Semu alitoa tahadhari kwa wananchi wanaotumia huduma za kuhamisha fedha kupitia simu za mkononi kwamba kuna matapeli wanaoghushi taratibu za huduma hiyo.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Kaimu Meneja Mahusiano kwa Umma, Semu Mwakyanjara alisema kumekuwa na ongezeko la matapeli wanaotuma ujumbe mfupi unaokaribia kufanana na ule wa watoa huduma.

“Upokeapo taarifa kuwa umetumiwa fedha kwa makosa na kufuatiwa na ujumbe mfupi unaofanana na ujumbe wa watoa huduma, kisha kutakiwa kurudisha fedha hizo, unachotakiwa ni kujiridhisha kwanza.

“Omba taarifa fupi ya akauti yako kwa watoa huduma ili uhakiki miamala yako na salio lako, ikibidi wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja,” alisema.

Mwakyanjara aliwataka wananchi kutotoa taarifa zozote kuhusu namba zao za simu au taarifa binafsi kwa mtu yeyote ambaye atawapigia simu.

“Ukipoteza simu au laini toa taarifa kwa watoa huduma na polisi na ukifanyiwa uhalifu na simu yako imetumika, toa taarifa ili wahalifu wasakwe,” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo