Taharuki ajali ya treni Ruvu


Suleiman Msuya

Ajali ya treni Ruvu
TRENI ya Shirika la Reli Tanzania (TRL) ambayo ilikuwa ikitokea mkoani Kigoma kwenda Dar es Salaam, imepata ajali katikati ya Stesheni ya Ruvu na Mgeta mkoani Pwani.

Mkurugenzi wa TRL, Masanja Kadogosa alithibitisha ajali hiyo akisema “Hapa nilipo naelekea katika eneo la tukio hivyo tukifika ndio tutajua kila kitu ndivyo ninavyoweza kusema ila ni kweli ajali imetokea.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Boniventure Mushongi alithibitisha ajali hiyo kutokea na kwamba wapo njia kuelekea katika tukio.

Alisema eneo ambalo ajali imetokea lina changamoto ya mawasiliano hivyo akifika huko ndio ataweza kutoa taarifa kamili.

Taarifa ambazo JAMBOLEO ilizipata zimeeleza kuwa katika ajali hiyo mabehewa saba yameanguka huku taarifa za kuwepo majeruhi viongozi wa TRL na jeshi la polisi wakisema hawakuwa na taarifa.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo