Walioongeza taa kwenye magari kukamatwa


Salha Mohamed
Mohamed Mpinga
JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, limeanza operesheni ya kukamata magari yenye taa zenye mwanga mkali ‘spot light’.

Operesheni hiyo itakayokuwa endelevu itahusisha magari yaliyoongezwa taa za ziada kwa kile kinachodaiwa kuwa ni urembo kwenye magari.

Uwekaji wa taa hizo ni kinyume cha sheria ya usalama barabarani kifungu cha 39 sura ya 168 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga, alisema jana kwamba utekelezaji wa operesheni hiyo unatokana na katazo alilitoa Desemba 22 mwaka jana.

“Nilisema kuwa hivi karibuni kumezuka mtindo wa kuweka taa zinazotoa mwanga mkali hasa kwenye vyombo vya moto kuanzia pikipiki hadi magari makubwa,” alisema.

Alisema taa hizo zimekuwa kero kwa madereva wengine na kusababisha ajali, hivyo aliwataka wamiliki wa magari kuzitoa kabla hawajayakamata.

Mpinga alisema madereva watakaokamatwa watachukuliwa hatua za kisheria, kwani tayari maelekezo yametolewa nchi nzima.

“Nimeshatoa maelekezo nchi nzima, kwamba kwa watakaokuwa wameweka taa kwenye magari makubwa, wengine huweka nyingi na kusababisha matatizo, kwani mwanga mkali hufanya dereva mwingine aache barabara na kusababisha ajali,” alisema.

Alifafanua kuwa wapo madereva wakimulikwa hupofuka kwa muda mfupi jambo linaloweza kusababisha ajali.

“Kama taarifa tulitoa muda wa kutosha tangu Decemba 22 hadi leo (jana) ni siku za kutosha kwa kutoa hadhari kwa wananchi,” alisema.

Alisema operesheni hiyo haitahusisha magari yaliyokuja na taa maalumu kutoka kiwandani pamoja na ya uwindaji.

“Kuna magari mengine huweka kwa sababu yanatumika kwa uwindaji, hayatahusika ila yanapoingia barabarani wanatakiwa kuzifunika

“Kuna mtindo wa magari makubwa kuweka taa kubwa nyuma zikimulika, mtu anayemfuata anaweza kufikiri gari linakuja kumbe linakwenda mbele,” alisema Mpinga.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo