Pigo la kwanza kwa Trump


Washington, Marekani

Rais Donald Trump
MAHAKAMA ya rufani nchini Marekani imetupilia mbali rufaa ya Rais Donald Trump kutaka kuendelea kutekelezwa kwa amri yake ya kuzuia wakimbizi, hasa kutoka kwenye mataifa ya Kiislamu kuingia nchini humo.

Kwa siku mbili mfululizo, miji miwili ya Washington na Minnesota ililaumu hatua hiyo ya Trump na wakaamua kwenda kufungua kesi kwenye moja ya mahakama mjini Seattle dhidi ya amri yake hiyo ya kuwazuia Waislamu.

Hata hivyo, Trump akishirikiana na timu yake ya haki na sheria waliamua kukata rufaa ya kupinga zuio hilo la mahakama wakishinikiza kuwa amri hiyo ya rais, iendelee kufanya kazi.

Mahakama imeeleza kuwa rufaa ya Trump ilikosa mashiko ya kikatiba na hivyo ikatoa siku moja hadi leo kuwasilishwa utetezi zaidi kuhusu nini wanakitaka katika rufaa yao.

Watu wenye pasi halali za kusafiria kutoka katika mataifa saba yaliyopigwa marufuku kuingia Marekani waliendelea kusota na kupata usumbufu licha ya mahakama kuweka zuio la kusitisha amri hiyo.

Amri ya Trump ambayo aliitoa mapema wiki iliyopita ilisababisha vurugu na maandamano makubwa kutoka kwenye maeneo tofauti duniani, ikiwemo Marekani katika miji kadhaa na viwanja vya ndege.

Juzi kulikuwa na maandamano makubwa katika miji ya Washington na Miami nchini Marekani na kwenye miji mingine kadhaa barani Ulaya.

Barani Ulaya maandamano hayo yameripotiwa kufanyika katika miji ya London, Paris, Stockholm na Barcelona. Hata hivyo, wakati watu hao wakiandaman kumpinga, wafuasi wa rais huyo mpya nao waliingie mitaani maeneo mbalimbali kumuunga mkono.

Tangu Trump asaini amri yake hiyo ya kuwazuia wakimbizi kuingia Marekani, tayari viza 60,000 zimefutwa au kuzuiwa kutolewa.

Hata hivyo, mara baada ya hakimu James Robert kutoa mwito wa kuomba vyombo vya sheria kuweka zuio la muda la kusitisha amri hiyo ya rais, mwito huo ulifanikiwa na amri hiyo kuwekwa pembeni kwa muda.

Trump alichukizwa na hatua ya Robert na kumtaka arudishe amri yake iendelee kufanya kazi.

Zuio la siku 90 aliloweka Trump liliwalenga wakimbizi na raia wa mataifa saba ya Kiislamu ambayo ni Iraq, Iran, Syria, Yemen, Somalia, Sudan na Libya.

Mashirika makubwa ya usafiri wa ndege bado yanawakubalia raia kutoka mataifa hayo husika, kusubiri ndege na kuingia Marekani.

Rufaa ilyokatwa na Serikali kupinga amri ya mahakama iliwasilishwa rasmi na kitengo cha haki na sheria cha Marekani.

Trump ametajwa kuwa ni mmoja kati ya waliokata rufaa hiyo sambamba na wengine kama vile Waziri wa Nyumba na Makazi, John Kelly pamoja Rex Tillerson.

Maelezo ya rufaa hiyo yanasema kuwa amri ya rais kukataza wakimbizi wasiingie Marekani ni kwa nia njema tu ya kutaka nchi kuwa salama.

Mbali na hivyo, Trump pia alionekana kuanzisha vita ya maneno dhidi ya hakimu, Robert kupitia mtandao wa twitter.

“Haya maoni ya kutoka kwa majaji yanayodai kutetea haki za binadamu ni ya kipuuzi dhidi yetu na kwa uwezo wetu tutayashinda,” alisema.

Trump aliongeza kuwa hawezi akafanya kazi na mahakimu ambao hawana uchungu na ulinzi wa taifa lao kwa kuruhusu kila mtu kuingia akieleza kuwa kufanya kufanya hivyo kutotoa fursa kwa wabaya na wema kuingia Marekani.

Alimalizia kwa kusema kuwa ana imani rufaa yao itashinda kitu ambacho kimekuja kuwa kinyume na matarajio.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo