Wadaiwa sugu kodi ya pango wapewa wiki mbili


Enlesy Mbegalo

Dk Yamungu Kayandabila
KATIBU wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Yamungu Kayandabila, ametoa siku 14 kwa wadaiwa sugu kulipa kodi ya pango ya Sh milioni 220, ikiwamo Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) ambayo inadaiwa Sh milioni 144.

Nyingine ni hoteli ya Lamada ambayo inadaiwa Sh milioni 54 na Tanganyika Motors ambayo inadaiwa Sh milioni 22.

Akizungumza na viongozi wa kampuni hizo Dar es Salaam  jana, katika oparesheni maalumu ya kukusanya kodi ya pango la ardhi kutoka kwa wadaiwa sugu wa kampuni, mashirika ya umma na watu binafsi kwa kuwafuata katika maeneo yao alisema yasipolipwa mali zao zitapigwa mnada.

“Katika hatua ya kwanza Wizara kwa kushirikiana na manispaa za mkoa wa Dar es Salaam imetoa notisi kwa wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi,” alisema Dk Kayandabila.

Pia alisema Serikali kwa kutumia kampuni ya udalali ya Msolopa Investment, itaendeleza oparesheni kwa kufika katika ofisi za wamiliki wa viwanja na mashamba makubwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Aliongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2016/17 Wizara ilipanga kukusanya Sh bilioni 111.77 kutokana na kodi ya pango la ardhi.

Alisema Wizara haitafanikisha malengo hayo endapo itaendelea kuwaachia wadaiwa sugu wasiotaka kulipa kodi.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo