Mbunge ahoji alipo Ben Saanane


Mwandishi Wetu, Dodoma

Pascal Haonga
MBUNGE wa Mbozi (Chadema), Pascal Haonga, amehoji bungeni juu ya kutoweka kwa Ben Saanane, ambaye ni msaidizi binafsi wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, na kutaka Serikali kueleza alipo.

Saanane alitoweka tangu Desemba mwaka jana na taarifa zake ziliripotiwa kituo cha Polisi Tabata jijini Dar es Salaam, ambapo hata familia yake ililieleza kuwa baada ya kumtafuta katika maeneo mbalimbali bila mafanikio, wameviachia vyombo vya dola kumfatuta.

Huku akitumia kanuni ya 68 (7) jana bungeni, Haonga aliomba mwongozo huo kwa Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, akihoji suala hilo, lakini uligonga ukuta kwa maelezo kuwa jambo hilo halikutokea bungeni siku ya jana.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, Saanane amepotea, hajulikani alipo lakini Serikali haioneshi jitihada zozote kama inavyofanya katika suala la kumtafuta Faru John,” alisema.

Huku akihoji nani mwenye faida kati ya faru John na Saanane, Haonga alisema hata Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, yuko kimya juu ya kutokewa kwa msaidizi huyo wa Mbowe.

Akitoa maelezo ya mwongozo huo, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge alisema: “Nadhani Haonga ulikuwa unataka kusikika tu, kwanza huyo Saanane sisi hatumjui, lakini Kanuni ya 68 (7) hairuhusu jambo hilo. Faru John sijui Saanane sijui ni kitu gani.”

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo