Lissu: Hakuna wa kunizuia urais TLS


Annastazia Maginga, Mwanza

Tundu Lissu
MGOMBEA urais Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ambaye pia ni mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amesema haki za kisheria zinamruhusu kugombea wafidha huo.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama mjini hapa juzi, Lissu alieleza kuwa uanachama wake TLS unatokana na ada alizolipa na anaruhusiwa kugombea kwani sheria haijakataza mwanasiasa kugombea.

“Watu wanaoleta hoja za mimi kutogombea kama ni wanasheria, basi hawajui kutumia uanasheria wao vizuri, kwanza hiki ni Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na si Tanzania Law Society.

“Ukiwa mwanachama wa chama cha wanasheria, unatakiwa kulipa kodi na ada na sheria hii haijakataza mimi kugombea eti kwa sababu ni mwanasiasa,” alisema Lissu.

Alieleza kuwa TLS kimepotea, kwani wao ndio wanaotakiwa kusimamia na kushughulikia haki lakini huenda anaogopwa kutokana na misimamo yake ya kikatiba.

“Ni wakati wa kuwa Rais wa TLS, ili kukisimamia chama hiki kwa kufuata haki kwa mujibu wa sheria na kukabiliana na  sheria mbovu zinazotungwa, mtu anayetakiwa kujua sheria kuliko mtu yeyote yule ni mwanasheria, wao ndio wanatakiwa kujua sheria zinasemaje,” alisema.

Alihadharisha kuwa endapo chama hicho kitafutwa, inamaana hakutakuwa na wakili na mambo yote yanayohitaji watu kama hao, hayatafanyika kwa kuwa mwanasheria katika nchi hii, ni lazima uwe mwanachama wa TLS.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo