…Vita vya mihadarati vyakolea



Salha Mohamed

MAPAMBANO yaliyoanzishwa ya kudhibiti dawa za kulevya Mkoa wa Dar es Salaam, yamechukua sura mpya baada ya jana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutaja watuhumiwa 65 wakiwamo wanasiasa, viongozi wa dini na kampuni.

Miongoni mwa wanasiasa wanaodaiwa kujihusisha na utumiaji na uuzaji wa dawa hizo ni Mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro, mbunge wa zamani wa Kinondoni(CCM), Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Askofu Josephat Gwajima na Diwani wa Mbagala (CCM), Yusuph Manji akiwataka kuwataka kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi kesho.

Hata hivyo, katika mkutano wake na wanahabari jana, Manji alisema atakwenda polisi leo, huku akieleza kuunga mkono vita dhidi ya dawa za kulevya, lakini akasema utaratibu uliotumiwa na Makonda umemvunjia heshima.

Kwa upande wake, Gwajima kupitia msaidizi wake Yekonia Bihagaze alisema wakati ukifika atatoa taarifa rasmi kuhusu tuhuma hizo.

Naye Mbowe kupitia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji alisema: “Chadema tunalaani kutajwa kwenye tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya kwamba si la kiungwana ni la kufedhehesha kwa viongozi.”

Akizungumza jana Makonda alisema Rais John Magufuli ameonesha dhahiri kutopendezwa na matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Alitaaja wamiliki wa Kampuni za mafuta na wamiliki kumbi za starehe na hoteli akiwataka kufika polisi kesho.

“Rais alielekeza vyombo vyote na wananchi kushiriki na kujenga taifa lenye usawa, nguvu kazi na lenye uchumi wa kati,”alisema.

Alisema wakati wanaanza kupambana na vita hiyo walianza kupita katika mitaa mbalimbali kuona namna ambavyo tatizo hilo ni kubwa na kuona namna watu walivyoathirika na dawa hizo.

“Wakati wa ziara ya Dar Mpya kuna mmoja alikuja kutuonesha namna tumbo lake lilipasuka baada ya vidonge kupasuka tumboni na kufanyiwa upasuaji,”alisema.

Makonda alisema kampeni hiyo ilianza kwa kutaja orodha ya wasanii na kuingia mtaani kwa kushuhudia ukubwa wa tatizo hilo na kupata taarifa sahihi.

Alisema mtu anapoitwa na Mkuu wa Mkoa anapewa haki yake ya kusikilizwa huku akibainisha kuwa kampeni hiyo si ya kwenda kimya kimya.

“Watu wanasema hii kitu ningeifanya kimya kimya lakini hapana kwani tulishafanya kimya kimya tangu mwanzo lakini tatizo linaendelea kuwa kubwa zaidi,’alisema.

Alilipongeza gazetu hili kwa kuonesha ushirikiano kwa wenyeviti wa serikali za mitaa kutoa majina katika mitaa yao ambao wanawasiwasi nao.

Aliwataka wenyeviti hao kutochoka na kutoa taarifa ndani ya siku kumi na kuanza mchakato wa awamu ya tatu kwa kupita nyumba hadi nyumba.

Alisema anatamani kuona mtoto wa shule ya msingi anaelewa kuwa dawa za kulevya ni hatari kwa afya yake pamoja na kuwabaini.

Alisema wapo vijana waliokiri kutumia dawa hizo na kuomba kusaidiwa kuacha dawa hizo ikiwemo msanii Khalid Mohamed (TID) na kukubali kuwasaidia.

“Baadhi yao hadi familia zao ilishaamua kuwatenga. Ninamaumivu makali sana ninapopita mtaani na kuona mateja wengi ambao wamezalishwa na watu wenye uchu wa utajiri wa haraka,”alisema.

 Alisema anaimani chini ya Rais Magufuli asiyekuwa na unafiki ataikisha nchi salama na dawa za kulevya kuwa historia katika serikali yake.

Makonda alifafanua kuwa zipo njia mbalimbalia ambazo amegundua hutumika kuigiza au kusafirisha dawa za kulenya kupitia Dar es Salaam.

“Nimekuwa operesheni usiku na mchana hatulali saa zote ili kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa salama. Imegundulika ipo sehemu ya kuingiza dawa kirahisi ambayo ni Dar es Salaam,”alisema.

Alisema watu hununua dawa kutoka Pakistani na kuja na meli ambayo inakuwa na mzigo na kuchukua boti zao kuingiza kwenye boti na kupakia kwenye mapipa ambapo meli inapokaribia bandarini huyatupa Zanzibar, Bagamoyo na Tanga yakiwa na GPRS.

“Wakija kwenye bandari zetu wanakuwa hawana dawa wakifika wanapakuwa mizigo yao kama kawaida halafu waliokubaliana huenda kwenye yale mapipa wakiwa na GPRS iliyofungwa nay ale mapipa na kuyaokoa na kuyachukua,”alisema.

Alisema baada ya kuyachukua huyaweka sawa na kuyasafirisha Afrika Kusini kupitia Mtwara.

“Njia ya pili hutumia magari kwa kununua Japan na kuzunguka nayo, wengine husafirisha kupitia meli za mafuta, wengine huwa na boti zao,’alisema.

Alisema wengine hutumia wasichana kwa kuwasafirisha nchini China akidai anachukua biashara nchini China.

Makonda alisema hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe katika kampeni ya kutokomeza dawa za kulevya, kwa mtu mwenye jina kubwa au dogo endapo taarifa zao zitakuwa na mashaka au kupata uchunguzi zaidi na kuwaachia wasiokuwa na hatia.

Alisema wapo waliokuwa nje ya nchi ambao walitakiwa kuripoti kituo cha polisi pindi watakapotua uwanja wa ndege wakamatwe.

“Wale waliokuwa wamejificha mahala tutawatafuta na tutawapata.Vita hii tukishindwa hajashindwa Makonda kwani wapo wanaodai kuwa hawezi,”alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo