NHC kumaliza kero ya makazi 2025



Georgina Misama, Maelezo

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), limejipanga kumaliza kero ya makazi ya nyumba kwa Watanzania ifikapo mwaka 2025.

Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC), Erasto Chilambo, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Ili kutimiza azma hiyo, Chilambo alisema nyumba zisizopungua 30,000 zitajengwa kwaajili ya kuuzwa na kupangishwa kwa watu wa kipato cha chini, kati na juu.

“Katika mkakati huu, Shirika limekusudia kujenga nyumba 12,000 kwa ajili ya watu wa kipato cha chini; nyumba 13,500 kwa ajili ya watu wa kipato cha kati na nyumba 2,700, kwa ajili ya watu wenye kipato cha juu,” alisema Chilambo.

Mbali na nyumba hizo za makazi, Shirika hilo pia litajenga majengo 1,800 ya kibiashara katika maeneo mbalimbali nchini, yanayotazamiwa kukamilika ifikapo 2025.

“Katika kuunga mkono uamuzi wa Serikali wa kuhamia Dodoma, shirika linajenga nyumba za makazi 300, zitakazouzwa kwa watumishi wa Serikali, ambazo zina ukubwa tofauti zenye vyumba 3 kila moja,” alisema Charahani.

Tangu kuanzishwa kwa NHC, imekuwa ikimiliki na kuuza majengo mbalimbali na hivi sasa shirika hilo linamiliki majengo 2,483 na maeneo 18,121 ya makazi na biashara katika mikoa ya Tanzania Bara.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo