Mbarawa aasa wanaohamia Dodoma


Mwandishi Wetu

Profesa Makame Mbarawa
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ametaka watumishi wa wizara hiyo katika sekta ya uchukuzi kutumia vizuri fursa ya kuhamia Dodoma kwa kutumikia Watanzania kwa uadilifu na weledi.

Mbarawa alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akiaga watumishi wa sekta ya uchukuzi wa awamu ya kwanza ambao wameondoka kwenda Dodoma.

“Nawapongeza kwa kupata fursa ya kuwa katika awamu ya kwanza katika wizara hii kuhamia Dodoma, fahamuni hii ni fursa na si changamoto, kwani hatua hii inasogeza huduma karibu na wananchi hivyo watumikieni kwa moyo,” aliwaasa.

Profesa Mbarawa alisema nia ya Serikali ni kuhakikisha watumishi wake wanahamia Dodoma na kuendelea na utekelezaji wa majukumu yake kwa wananchi.

Katibu Mkuu, Dk Leonard Chamuriho alisema awamu ya kwanza ya watumishi zaidi ya 45 inahamia Dodoma mwezi huu na awamu ya pili itaanza Machi na watumishi wote wa sekta ya uchukuzi watakuwa Dodoma Agosti.

“Watumishi wa Sekta ya Uchukuzi wanaohamia Dodoma katika awamu ya kwanza ni pamoja nami, wakurugenzi na wakurugenzi wasaidizi, wakuu wa vitengo na maofisa waandamizi,” alisisitiza Dk Chamuriho.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo