Akamatwa akidaiwa kumuingilia mbuzi


Aidan Mhando, Mwanza

JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia mkazi wa Mabatini Wilaya ya Nyamagana, Jumanne Nassib (20), kwa tuhuma za kukamatwa akifanya mapenzi na mbuzi vichakani.

Akizungumzia tukio hilo juzi, Kamanda wa Polisi, Ahmed Msangi alisema lilitokea Februari 8, mwaka huu na   mmiliki wa mbuzi alifahamika kwa jina la Benedictor Bunga (33).

Kamanda alisema mwenye mbuzi alikwenda kuwafunga kwenye malisho mbuzi wake sita na alipokwenda kuwaangalia aliwakuta wakiwa watano.
“Saa tatu asubuhi mmiliki wa mbuzi alikwenda kuwaangalia kwenye malisho alikowafunga kwa ajili ya chakula na kukuta wakiwa watano. Alipatwa na mshtuko akaanza kumtafuta vichakani,”alisema Msangi.

Alisema wakati akiendelea kumtafuta ghafla mtuhumiwa alionekana akimuingilia mbuzi aliyepotea ambapo mmiliki wa mbuzi alipiga kelele kuomba msaada na hatimaye kukamatwa.

“Mtuhumiwa yupo Polisi na mahojinao yanaendelea kuhusu tuhuma zinazomkabili kwani jambo alilofanya ni kosa kisheria. Utaratibu unafanyika ili kumpeleka mtuhumiwa hospitali kuangaliwa kama ana akili timamu au la na uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani,”alisema.

Msangi aliwataka wakazi wa Mwanza kutoa taarifa wanapoona kuna mtu mwenye tabia kama hizo kwani hazikubaliki ndani ya jamii.


Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo