Serikali kuajiri walimu 4,000 wa Sayansi


Sharifa Marira

Profesa Joyce Ndalichako
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, amesema Serikali inatarajia kuajiri walimu wa masomo ya Sayansi zaidi ya 4,000 ili kupunguza uhaba wa walimu hao nchini.

Profesa Ndalichako alisema hayo juzi kwenye ziara yake wilayani Rufiji akieleza kuwa kipaumbele kitatolewa kwa shule za wilaya hizo, ambazo kila aliyotembelea alikuta uhaba wa walimu hao na zingine kutokuwa nao kabisa kwa miaka zaidi ya mitano.

Akiwa katika Sekondari Utete akifuatana na Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa (CCM) alieleza kusikitishwa na kufeli kwa wanafunzi wengi wa kidato cha nne mwaka jana na kuwaeleza kuwa Serikali itajitahidi kutatua changamoto zilizopo ili wanafunzi wasipate kisingizio cha kufeli.

“Jitihada za Mbunge wenu anavyowaongelea bungeni, zimenileta hapa leo kutokana na Serikali kuwa sikivu lakini nimesikitishwa na matokeo yenu ya mwaka jana, mmefeli sana lakini nimeona changamoto zilizopo shuleni kwenu ukiwamo ukosefu wa walimu hasa wa Sayansi, kuhusu vifaa vya maabara tutawaletea mwezi huu na uchakavu wa vyoo tutajitahidi kurekebisha,” aliahidi Ndalichako.

Aliasa wanafunzi kutochanganya mambo na kuendekeza ngoma, muziki au mapenzi kwani mambo hayo yanachangia kiasi kikubwa wanafunzi kufeli.

Mchengerwa aliwataka wanafunzi kujibidiisha na masomo kwa kuwa katika kipindi cha uongozi wake anajitahidi kuishawishi Serikali kuboresha elimu ili kuzalisha wasomi wengi ambao wataendeleza wilaya yao.

Aliipongeza serikali kwa kusajili shule ya Umwe ambako wanafunzi walikuwa na shida kusoma shule mbili tofauti kwa kuwa hawakuruhusiwa kufanya mitihani katika shule ambayo haijasaliwa na kilichobaki ni kuboresha miundombinu ya shule hiyo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo