Mamlaka ya dawa za kulevya yapata bosi


Mwandishi Wetu

Rais John Magufuli
BAADA ya Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kukaa kwa muda mrefu bila Kamishna Mkuu, hatimaye amepatikana.

Bosi huyo wa Mamlaka hiyo anakuja huku kukiwa na sekeseke la watu mashuhuri wakitangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwa wanajihusisha na mihadarati.

Jana Rais John Magufuli alimteua Rogers Sianga kuiongoza Mamlaka hiyo kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa.

Kwa mujibu wa uteuzi huo wa Rais, Kamishna Mkuu Sianga atasaidiwa na Mihayo Msikela ambaye anakuwa Kamishna wa Operesheni.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Fredrick Kibuta ameteuliwa kuwa   Kamishna wa Intelijensia.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dk Anna Makakala kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.

Kabla ya uteuzi huo, Dk Anna alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji Moshi, mkoani Kilimanjaro.
“Uteuzi huu unaanza mara moja na wateule wote wataapishwa Jumapili   saa 5 asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam,” ilieleza taarifa hiyo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo