Makonda apania Dar kuwa ya kitalii


Suleiman Msuya

Paul Makonda
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema wako katika mchakato wa kubadili vivutio vilivyoko mkoani humo  kuwa vya kitalii ili kuchochea ukuaji uchumi.

Makonda alisema hayo jana wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya ujio wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kesho huku Rais wa Shelisheli, Danny Faure akija  Februari 27.

Makonda alisema Dar es Salaam imekuwa ikipokea viongozi wengi kutoka ndani na nje ya nchi, hivyo ni wakati mwafaka sasa kuangalia fursa za kitalii zilizopo.

Alisema Jiji lina vivutio vya asili na visivyo vya asili na baadhi ya visiwa vikitumika ipasavyo vitachangia uchumi na maendeleo kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa alitaja baadhi ya maeneo kama sanamu ya askari, jengo la Karimjee na mengine mengi yakitumiwa vizuri ni chanzo sahihi cha mapato.

“Tumekuwa tukipokea viongozi kutoka nje na ndani ya nchi na wananchi lakini ukweli hatujatumia vivutio vilivyopo kuwa kichocheo cha mapato ya Jiji,” alisema.

Alisema wakati wa kuifanya Dar es Salaam kama njia umepita   hivyo atahakikisha anafanikisha lengo hilo la kuibadili kuwa Jiji la kitalii.

Makonda alisema pamoja na kulibadilisha kwa kutumia fursa za kitalii pia anatarajia kuona wananchi wakifaidika moja kwa moja kwa kuuza bidhaa kwa wageni watakaokuja kulitembelea.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo