Iddi Azan, mmiliki Casino Sea Cliff wahojiwa

Celina Mathew

Iddi Azan
ALIYEKUWA Mbunge wa Ilala, Iddi Azan na Mmiliki wa Sea Cliff Casino, wamekwenda kuripoti kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda.

Juzi Mshauri Mkuu wa Kampuni ya Quality Group, Yusuph Manji na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gawajima walikuwa wa kwanza kuripoti kituoni hapo kama walivyoahidi.

Makonda alitaka watu 65 wakiwamo hao kuripoti kituoni hapo na kukutana na Kamati ya Upelelezi iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa huo, ili wahojiwe kuona kama wanahusika na dawa za kulevya au la.

Licha ya Manji na Gwajima kuripoti juzi, jana saa 3:06 gazeti hili lilishuhudia Azan akiwasili akiwa na gari aina ya Jeep kuhojiwa akifuatana na baadhi ya watu wake wa karibu.

Aidha, saa 10:25 mmiliki wa Sea Cliff Casino aliwasili kituoni hapo akiwa na gari namba T 356 DHU aina ya Noah na baadhi ya watu ambao walimbebea kiti cha kukalia kwa kuwa ni mzee.

Akizungumzia waliofika juzi na jana kwenye kituo hicho ambao ni wanane, Kamishna wa Kanda hiyo, Simon Sirro  alisema operesheni hiyo inaendelea vizuri na kushukuru  wana Dar es Salaam ambao wanaendelea kutoa taarifa kuhusu masuala hayo ili kuondokaa na uhalifu wa aina hiyo.

“Hadi jana kati ya watu 65 waliotakiwa kuripoti kituoni hapo kwa ajili ya kuhojiwa, ni wanne akiwamo Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajina na Mshauri Mkuu wa Kampuni za Quality Group, Yusuph Manji ambao jana (juzi) waliripoti na upelelezi uliendelea hadi usiku.

“Wamelala mahabusu na unaendelea kufanyika, kimsingi agizo ninalotoa kama Makonda alivyosema, wahusika wajitokeze kwa kuwa ofisi ya upelelezi iko wazi,” alisema.

Kamishana Sirro alisema kwa sasa hawezi kuweka wazi majina ya waliohojiwa na kueleza kuwa waliotajwa wanapaswa kuacha uoga wajitokeze.

Alisema wanaojihusisha na vitendo hivyo wataendelea kubaki mahabusu na watakaoonekana hawahusiki, wataachwa  na kusisitiza kwa ambao hawajafika wafike.

“Huna sababu ya kuwa na uoga maana watu wanapiga simu sana mmefanya nini na wengine wanatuma ndugu zao, hivyo huna sababu ya kumtuma ndugu yako kuja kumwona Sirro, suala la msingi umetajwa na unajua ni msafi huna makandokando, ripoti kwenye Kamati itakuhoji na kupeleleza mambo yote ikiona huhusiki itakuacha,” alisema.

Alisema kimsingi hadi sasa baadhi ya watu wameripoti na ataelezea zaidi kesho (leo) na kwamba wengine wanaendelea kufika kituoni hapo kuonana na timu ya upelelezi.

Katika hatua nyingine, alisema kwenye mwendelezo wa  operesheni dhidi ya wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya, Jeshi  hilo  limekamata watuhumiwa 11 wakiwa na kete 38 za bangi na magunia sita ya bangi.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo