Ujenzi daraja la Ubungo waiva


Suleiman Msuya

WAKALA wa Barabara Tanzania (Tanroads), umetiliana saini ya ujenzi wa daraja la Ubungo na Kampuni ya China Civil Engeneering Constraction Corporation (CCECC), ambao unatarajiwa kuanza mwezi ujao na kugharimu zaidi ya Sh. bilioni 177.

Utiaji saini huo unakuja siku chache baada ya Rais John Magufuli kumuomba Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (WB) upande wa Afrika, Makhtar Diop kusaidia ujenzi huo wakati wa uzinduzi wa usafiri wa mabasi ya mwendokasi.

Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Mhandisi Patrick Mfugale alibainisha hayo alipozungumza na waandishi wa habari jana baada ya utiaji saini makubaliano hayo makao makuu ya wakala huo jijini Dar es Salaam, huku ikibainishwa jengo la Makao makuu ya Tanesco halitaguswa na ujenzi wa daraja hilo la ghorofa tatu.

Mfugale alisema makubaliano yao ni kuwa ujenzi uanze kuanzia sasa na utadumu kwa miezi 30 ili kuondoa changamoto ya foleni kwenye eneo la Ubungo.

Alisema WB imetoa mkopo huo ambapo mkandarasi atalipwa moja kwa moja na Sh. bilioni 8.2 atalipwa mhandisi mshauri kwa ajili ya usimamizi ambaye ni Kampuni ya M/s Dasan ya Korea Kusini ikishirikiana na Kampuni ya Afrika Ltd ya Tanzania.

"Tumetiliana saini ujenzi wa Daraja la Ubungo ‘interchange’ na Kamapuni ya CCECC ambapo zaidi ya Sh.bilioni 177 zitatumika na litakuwa daraja la ghorofa tatu ni kazi ya miezi 30," alisema.

Mfugale  alisema safu ya chini ya daraja hilo itatumika kwa magari ya Barabara ya Morogoro na kupinda kushoto na safu ya pili itajengwa katika urefu wa mita 5.75 kutoka usawa wa ardhi  na itatumika kwa magari yote yanayopinda kulia na kuongozwa taa za barabarani.

Alisema Safu ya tatu itajengwa kwa urefu wa meta 11.5 kutoka usawa wa ardhi na itatumika kwa magari yanayopita Barabara za Mandela na Sam Nujoma na barabara zote zitakuwa na njia sita.

Mtendaji huyo alisema kampuni 48 ziliomba zabuni ila ni 14 ambazo zilirejesha hivyo baada ya kupitia kwa makini CCECC ilifanikiwa kushinda.

Alisema upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ulifanywa na Kampuni ya M/s Hamza Associates ya Misri kwa kushirikiana na Kampuni ya Advanced Engineering Solutions Ltd ya Tanzania kwa gharama ya zaidi ya sh. milioni 951 ambapo kazi ilikamilika Desemba 2016.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo