Upasuaji figo kuanza mwezi ujao


Salha Mohamed

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), inatarajia kuanza rasmi upasuaji wa kupandikiza figo Machi.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili jana Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma cha MNH, Aminiel Aligaesha alisema kwa sasa wapo kwenye maandalizi ya kutoa huduma hiyo.

Alisema huduma hiyo ilipaswa kuanza Januari au Februari, lakini kutokana na kutokamilika kwa vifaa na ukarabati hospitalini hapo haikuwezekana.

“Hatuwezi kuanza ukarabati ukiwa bado na baadhi ya vifaa lazima zifuatwe,” alisema.

Alisema madaktari bingwa wa upasuaji waliokwenda kujifunza walirudi Desemba mwaka jana.

Aligaesha alisema kutokana na hali hiyo, hospitali inaendelea na maandalizi ya kutoa huduma hiyo, na hadi sasa wataalamu 18 wa fani mbalimbali wamejengewa uwezo wa upandikizaji figo kwa wenye matatizo hayo.

Sambamba na hilo, Aligaesha alisema huduma ya upandikizaji wa kifaa cha usikivu kwa watu wazima na watoto utaanza rasmi Machi.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo