Wateja simu za mkononi wapungua

Mwandishi Wet

RIPOTI ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya Desemba mwaka jana imebaini kuporomoka kwa idadi ya wateja wa kampuni za simu nchini.

Hata hivyo imebainisha kuwa kampuni ya Vodacom Tanzania pekee ndiyo imezidi kupata wateja wengi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, idadi ya watumiaji wa huduma za simu za mkononi imepungua kutoka 40,560,368 Novemba mwaka jana hadi 40,173,783 Desemba wakipungua wateja 387,000.

Ilibainishwa kuwa pamoja na upungufu huo wa wateja, Vodacom imeendelea kupata wapya ikisajili 64,951 na kuongezeka kutoka 12,354,474 hadi 12,419,425.

Tigo ina wateja  11,677,344 huku Airtel ikiwa na asilimia 26 ya soko la watumiaji simu na kampuni mpya ya Halotel ikifikisha idadi ya wateja 11,020 katika kipindi hicho.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika robo ya mwisho ya mwaka jana matumizi ya simu yaliporiomoka ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka juzi.

Kwa upande wa matumzi ya huduma za kifedha kupitia simu za mkononi, ripoti ya TCRA ilibainisha kuwa hadi mwishoni mwa mwaka jana, huduma ya M-Pesa ya Vodacom iliongoza katika soko kwa asilimia 45, Tigopesa asilimia 52.6 na Airtel Money asilimia 40.3.

Akizungumza kuhusu ripoti hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom,  Rosalynn Mworia alisema ni fahari kwao kuona bado wanakubalika kwa Watanzania wengi na kuendelea kuwa kinara wa kampuni za mawasiliano nchini katika robo ya mwisho ya mwaka jana licha ya changamoto zilizopo kenye masoko.

“Mafanikio haya yanadhihirisha kuwa tunaongoza kwa kubuni na kutoa huduma bora zinazokwenda sambamba na mahitaji ya soko la mawasiliano, na dhamira yetu ya  kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidigitali kupitia ubunifu wa  teknolojia ya mawasiliano, ili kukidhi haja za wateja wetu,” alisema Mworia.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo