Waziri Mkuu aagiza CAG achunguze ATCL


Mwandishu Wetu

Kassim Majaliwa
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema atamwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuchunguza ukusanyaji mapato ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).

Alitoa kauli hiyo jana alipotembelea makao makuu ya shirika hilo Dar es Salaam kwa lengo la kujionea mwenendo wa uendeshaji wake.

“Nitamwagiza CAG aje aangalie mwenendo wa ukusanyaji wa mapato ya shirika hili kuanzia mwaka jana lilipoanza kufanya kazi hadi sasa,” alisema.

Waziri Mkuu alisema Serikali haiko tayari kuona shirika hilo linakufa tena, hivyo aliwataka viongozi wake wahakikishe linaendeshwa kwa mafanikio kwa manufaa ya Taifa.

Pia aliwataka waache kukusanya mapato kwa kutumia risiti za kuandika kwa mkono na badala yake waanze kutumia mfumo wa elektroniki ili kuzuia upotevu wa mapato hayo.

“Vitu vingi vinavyokwenda manual ni rahisi kufa. Serikali tumeagiza malipo yote yafanyike kielektroniki na kote tunakotumia mfumo huu tumepata mafanikio,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa ATCL, Witness Mbaga ajiridhishe na fedha zinazokusanywa katika eneo la mizigo kama ziko sahihi, lengo ni kudhibiti upotevu wa mapato.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alitaka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha wanazingatia ratiba ya njia na muda wa safari ili wasipoteze wateja.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo