Mito 80 Kilombero hatarini kukauka


Leonce Zimbandu

MITO 80 iliyokuwa ikitirisha maji misimu yote katika wilaya ya Kilombero, ipo hatarini kukauka.

Aliyekuwa Mbunge wa Kilombero, Abdul Mteketa alisema hayo jana alipozungumza na mwandishi wa gazeti hili na kulaumu  jamii ya wafugaji na wakulima kwa kuharibu mazingira ya vyanzo vya maji ya mito hiyo.

Mteketa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mazingira katika wilaya hiyo, alisema baadhi ya wafugaji wamekuwa wakinywesha mifungo maji kuharibu na kingo za mito hiyo na vyanzo vyake vya maji, huku baadhi ya wakulima wakilima kado ya mito hiyo.

Kwa mujibu wa Mteketa, hata baadhi ya viongozi wa wilaya hizo wasio waaminifu, wamechangia hali hiyo kwa kutoa ruhusa ya kufanyika kwa uharibifu huo.

Alisema haiwezekani mtu alime kwenye vyanzo vya maji na mifugo iachiwe izagae hovyo kwenye mabwawa na mito bila kuchukuliwa hatua madhubuti.

“Naomba viongozi na wananchi wa wilaya ya Kilombero wawe   makini katika utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji,” alisema.

Alisema kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa Mazingira, anapaswa kupaza sauti ili hatua madhubuti za kutunza mazingira zichukuliwe katika Mto Kilombero ambako kunapatikana mnyama aina ya Puku.

Alisema ikiwa juhudi hazitachukuliwa kudhibiti mifugo na wakulima kando ya kingo za mito hiyo, baada ya miaka kadhaa Mto Kilombero utakauka na kusababisha jangwa.

Mteketa alisema hata mkoa wa Morogoro kuchaguliwa kuwa ghala la chakula, kulitokana na bonde la Mto Kilombero, hivyo tahadhari isipochukuliwa hata jukumu la mkoa huo la kuwa ghala la chakula litashindikana.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo