Watanzania 50 watimuliwa Msumbiji


Sijawa Omary, Mtwara
Rose Mhagama
WATANZANIA zaidi ya 50 wakiwamo watoto wamefukuzwa

Kituo cha Uhamiaji cha Kilambo hivi karibuni kilipokea raia hao huku ikidaiwa kuwa walilazimishwa kuondoka nchini humo bila sababu za msingi wakati walikuwa wakiishi kwa kufuata taratibu zote za kisheria.

Naibu Kamishna wa Uhamiaji na Ofisa Uhamiaji wa Mkoa, Rose Mhagama, alisema raia hao walipokewa kituoni hapo juzi saa 11 jioni baada ya kufika kituoni hapo bila kufuata utaratibu wa kawaida.

Alisema Watanzania hao walilalamika kunyanyaswa, kupigwa, kuporwa mali, kulazwa mahabusu kwa siku tatu bila msaada wa chakula wala kupewa nafasi ya kujieleza.

Raia hao walikaguliwa na kuhojiwa ili kupata taarifa zao  za muhimu  ili wawe maeneo ambayo wanaweza kupatikana kirahisi nchini.

“Lakini sisi Serikali tunataka kuona jinsi tunavyoweza kufanya ili kurudishiwa mali zao lakini pia tukilinda uhusiano baina ya nchi zetu,” alisema Mhagama.

Alisema Uhamiaji imetekeleza wajibu wake wa kuwapokea kutokana na mazingira waliyokuja nayo kuwa magumu, baada ya kuporwa mali jambo ambalo limeleta picha mbaya kwa ujirani mwema na ni ukiukwaji wa haki za binadamu.


“Kwa umoja wetu tuliwachangia kiasi tulichoweza ili kuwawezesha angalau kufika Mtwara baada ya wao kusema wakifika hapa itakuwa rahisi mawasiliano na ndugu zao kufanyika huku taratibu zingine zikiendelea,” alisema Mhagama.

Kwa mujibu wa raia hao, wako zaidi ya 60 na waliiomba Serikali ya Msumbiji iwasaidie kupata haki zao ikizingatiwa kuwa wako nchini humo kwa kufuata taratibu husika huku wakishangazwa kuona raia wa nchi hiyo wakiwa nchini kwa amani.

Matilda Mwakipesile wa Mbeya ambaye yuko nchini humo kwa miaka sita hivi sasa ambaye alikuwa ni mjasiriamali mdogo aliiomba Serikali ya Tanzania iwasaidie kupata mali zao kwa kuwa hawajui kosa lao hadi kunyanyaswa.


“Watanzania wako wengi hapa kwetu Tanzania na wanaishi kwa amani bila nyanyaso mbona sisi hatuwanyanyasi … tunamwomba Rais wetu atusaidie kupata haki zetu na tuko Msumbiji kwa kuwa tuna vielelezo vyote vinavyotakiwa,” alisema Mwakipesile.

Augustino Mayamba wa Dar es Salaam ambaye yuko nchini humo kwa miaka minne sasa, alisema watu walifika nyumbani kwake na kumtaka aende kwenye mkutano huku wakimtishia kumuua.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo