Sumaye, Lowassa watabiriwa kurudi CCM


Mwandishi Wetu

MTABIRI maarufu nchini, Hassan Hussein ametabiri mambo 20 yatakayojiri mwaka huu 2017, ikiwemo viongozi walioikimbia CCM na kujiunga na upinzani kurejea kwenye chama hicho tawala.

Ingawa Hussein hakuwataja viongozi hao, waliotikisa walipotangaza kung’atuka CCM ni waliokuwa mawaziri wakuu kwa nyakati tofauti; Edward Lowassa na Frederick Sumaye.

Lowassa aliihama CCM baada ya kukatwa kwenye mchakato wa kuwania urais kupitia chama hicho mwaka juzi na hivyo kujiunga na Chadema ambako alipitishwa kuwania urais akiungwa mkono na vyama vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Sumaye aliungana na Lowassa baadaye na akachaguliwa kuwa meneja wa kampeni za mgombea huyo aliyeshindana vikali na aliyekuwa mgombea wa CCM kwenye uchaguzi huo, John Magufuli.

Mbali na utabiri huo, Hussein alisema hali ya uchumi itaimarika zaidi mwaka huu na hali ngumu ya maisha iliyokuwepo mwaka 2016 itatoweka.

Aidha, amemtabiria Rais John Magufuli kupata nishani ya juu ya dunia kutoka kwa Rais wa moja ya mataifa makubwa duniani kutokana na uongozi wake, huku akitabiri viongozi waliokimbia chama tawala CCM na kwenda upinzani, watarejea.

Maalim Hussein ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mtabiri maarufu, marehemu Sheikh Yahya Hussein, katika utabiri wake wa mwaka 2017 ametabiri mambo 20 kutokea nchini likiwamo la viongozi wengi wa kisiasa na kidini kukumbwa na kashfa ya ngono na wengine kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na kashfa za kiuongozi.

Alisema mwaka huu umeanza siku ya Jumapili na kwa mujibu wa utabiri siku hiyo inashabihishwa na sayari ya jua ambapo kinyota yake ni Simba, ambayo asili yake ni moto.

Pia huonesha kuwa nia ya ufalme , utawala na uongozi wa dini na kisiasa."Sayari hii inahusika na kiburi, kutumia nguvu, ufahari, kuona haya, mambo ya kisiasa, udereva kwa maana vyombo vya moto na mambo ya ufundi magari.

"Mwaka unapoanza Jumapili unaonesha kuwa utakuwa baridi, yaani hautakuwa na rabsha nyingi lakini  hautaki uharaka wa mambo.Kikubwa kuliko vyote ni kwamba mambo huenda pole pole na yanahitaji subira kwa wale wanotaka mafanikio,"alisema.

Maalim Husseina aliongeza mwaka unapoanza Jumapili  au kutumia tangaza utabiri huo jijini Dar es Salaam jana, Maalim Hussein ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mtabiri maarufu Afrika Mashariki mara nyingi wa kijicho, watu na hasa wanasiasa, viongozi wa dini na wa familia kuoneana husda na watu kada hiyo hujikuta wakikumbwa na vifo vya kawaida au vya kuuawa na kuuana.

Alieleza kutokana na hali hiyo mwaka 2017 utakuwa mgumu wa mambo, mabishano ya kisiasa, kijamii na mataifa mbalimbali kuhasiamiana,

Alisema kutokana na mwaka huu ulivyo kinyota mambo mengine ambayo anatabiri kutokea ni kuzama kwa meli kwenye moja ya habari kuu za dunia na ndege moja ya taifa kubwa duniani kuanguka na hivyo kusababisha vifo vya watu kadhaa.

Pia ametabiri kutokea mvutano wa kimtazamo na sera utakaosababisha mabadiliko makubwa ya uongozi wa serikali duniani na Tanzania ikiwamo ambapo baadhi ya wanasiasa watapotea kabisa katika uliongo wa siasa.

Maalim Hassan alitabiri viongozi wa dini kutoa matamshi ya kutatanisha ambayo yanaweza kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani na utulivu.Pia ametabiri muanguko wa vyama vya tawala katika nchi mbalimbali duniani.

Pia ametabiri kutokea ajali nyingi ambazo zitawakuta wanasiasa, watawala na viongozi wa dini katika mwaka 2017 na kufafanua wimbo la vifo lililoikumbuka tasnia ya habari mwaka 2016 duniani kuendelea kwenye mwaka huu wa 2017.

Maalim Hassan alitabiri vifo vya ghafla vya kawaida vya wasanii maarufu duniani na Tanzania ikiwamo na vinaweza vikatokana na fumanizi, kuuliwa na kuana wenyewe.

Pia ametabiri kuwa mwaka 2017 utakuwa ni mwaka wa mabadiliko makubwa katika tasnia tofauti za kisiasa, kimichezo,kidini na kiburudani kwa maana ya kwamba wale waliokuwa wakiongozwa au kunawiri katika sekta hizo kushindwa katika chaguzi zao, kuondolewa kwa nguvu au kukataliwa na watu.

Katika utabiri wake Maalim Hassan alitabiri kifo cha chama kimoja maarufu cha siasa hapa nchini.Hata hivyo hakutaja ni chama gani licha ya kufafanua kuwa CUF iko kwenye migogoro lakini si lazima kiwe chama hicho.

"Maana wapo wanaweza kudhani amekitabiria lakini ukweli kwenye utabiri huwa halengi mtu au kutaja jina ila watanzania wasubiri kuona matokeo ya utabiri wake na kueleza katika miaka sita ya kuifanya kazi hiyo kila ambalo anatabiri basi linatokea kwa asilimia zaidi ya 96,"alisema.

Alisema mwaka huu utabiri wake unaonesha CCM kushika hatamu zaidi itakayoleta maendeleo makubwa kwa chama hicho na nchi ya Tanzania kwa ujumla.

Maalim Hassan alipotakiwa kuwataja viongozi gani waliondoka CCM na kwenda upinzani na sasa anwatabiria kurudi ni akina nani hakuwa tayari kutaja majina yao.

Alisema kwenye utabiri wake hataji mtu ingawa anajua wapo viongozi kama Edward Lowasa(Waziri Mkuu wa zamani), Kingunge Ngombari-Mwiru , Hamisi Mgeja, Laurance Masha na wengine wengi waliondoka CCM na kwenda upinzani.

"Najua wapo watakaoanza kuwataja viongozi hao, lakini niseme tu katika kutabiri huwa sitaji mtu wala kumlenga mtu, hivyo tunatakiwa kusubiri kuona haya ambayo nimebari na kila ninapotabiri huwa nafuatilia ili kujua yapi yametokea na yapi hayakutokea,"alifafanua Maalim Hassan.

Kuhusu utabiri wake kuonesha mafanikio makubwa kwa Serikali ya Rais John Magufuli alisema, Rais ni kiongozi wa nchi hivyo utabiri ukionesha mema au mabaya lazima ayaseme kwa kutaja jina lake maana anawahusu Watanzania wote.

"Katika utabiri nimezungumzia mafaniko ya Rais Magufuli kwa kutaja jina lake na kwa nafasi yake lazima ninapotoa utabiri unamhusu yeye nitaje jina lake ingawa kwa wengine siwezi kutaja majina yao bali naeleze kile ambacho kinaonekana katika utabiri,"alisema Maalim Hassan.

Alishauri kuwa vifo na maafa ambavyo ametabiri vinaweza visitokee iwapo watu wataacha rabsha na uharaka wa kufanya mambo kama nyota ya mwaka 2017 inavyosema.Pia watu waache chuki binafsi, choyo, kuchonganisha na ngono isiyokubalika kisheria katika masuala ya siasa, jamii, utawala na mamlaka.

Alipoulizwa vipi kuhusu waandishi wa habari ambao waliandika habari zinahusu Mchungaji Lusekelo kudai waandishi walimuandika watakufa, Maalim Hassan alisema hakuna mwandishi atafariki dunia kwasababu ya kumuandikia mchungaji huyo ila ni matokeo ya kuelekea kwenye anguko lake.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo