Leonce Zimbandu
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) linatarajia kupiga mnada
mali za Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iwapo
atashindwa kulipa deni la sh. Bilioni 1.172 kwa muda wa siku 14.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya NHC kufuata taratibu zote za kisheria
kwa kutoa notisi ya siku 30 na kumalizika Agosti 29, mwaka huu na lakini
mdaiwa alishindwa kulipa deni hilo.
Jana majira ya saa 07:00 NHC wakiwa na
Kampuni ya udalali ya Fosters Action Mart walifika katika Ofisi za
gazeti la Tanzania Daima na Club ya usiku ya
Bilicans na kutoa dhamani za ofisi nje ya jengo hilo.
Meneja wa Ukusanyaji kodi wa NHC, Japhet Mwanasenga
aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa kutoa nje thamani
hizo jijini Dar es Salaam jana.
Alisema mpango
huo kuwaondoa kwenye nyumba wadai sugu
siyo kwa Mbowe pekee bali wengine
wanapaswa kujiandaa kwa kulipa
mapema kodi hiyo kabla ya rungu la sheria halijawafikia.
“Tumeanza kumdai kodi ya pango Mbowe
tangu mwaka 1995 na kupewa muda wa
kulipa lakini ameshindwa kulipa, hivyo
kilichobaki ni utekelezaji na suala hili halina siasa hata taasisi za serikali
zinazodaiwa hatua zitachukuliwa, ikiwamo kuwaondoa,” alisema.
Alisema Mbowe ni
mpangaji kama wapangaji wengine wala hana
ubia na shirika hilo, kama ingekuwa hivyo angeendeleza kwa kujenga Mbowe Hoteli kama alivyojitambulisha kwenye Mkataba.
Mwanasenga aliendelea kusema kuwa hilo siyo suala la
kisiasa bali ni suala la kiutendaji kwa
ajili ya kukusanya madeni yote iwe kwenye taasisi za serikali au binafsi.
Mkurugenzi wa
Kampuni ya Udalali ya Fosters Actionn Marts, Joshua Mwaituka
alisema kwa mujibu wa sheria yam waka
2005 inatoa fursa kwa NHC kumwondoa Mpangaji wake ikiwa atashindwa kutimiza
masharti ya mkataba.
Alisema wakiwa madalali
wanaendeleza kufuata maelekezo ya mteja wao, hivyo watasubiri siku 14
zimalizike ili waanze kuuza mali hizo.
“Thamani zote za Mbowe zilizopo katika jengo la Mbowe
Hoteli zipo chini ya Kampuni yangu kwa kuuzwa ikiwa mdaiwa atashindwa
kuvikomboa ndani ya siku alizopewa,” alisema.
Agosti 24, mwaka huu Mbowe alisema amepata taarifa ya
mkutano wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Waandishi wa
habari kuhusu kilichoitwa “wadaiwa sugu” wa NHC ambapo katika orodha hiyo
kampuni ambayo ina hisa ya Mbowe Hotels Co.Ltd imeorodheshwa kama mdaiwa
anayedaiwa zaidi ya Shilingi Bilioni moja.
Alikiri kuwapo kwa mgogoro wa kibiashara wa miaka mingi
baina ya Kampuni hii na NHC lakini alisema kampuni hiyo imekuwa ikilipa kodi
stahiki kwa NHC kwa mujibu wa makubaliano yao ya kibiashara.
Mbowe alidai kumekuwepo na ukakasi wa muda mrefu
kuhusiana na mkataba wa umiliki,
uendelezaji na uendeshaji wa jengo hili unaochagizwa na msimamo wake wa
kisiasa.
Haki na Uhuru wa
kufanya biashara kama raia wengine umekuwa ukiingiliwa mara kwa mara katika
mazingira yanayoambatana na vitisho kiasi ambacho maamuzi kadhaa hayafanyiki
kwa hofu ya kisiasa
Hivyo, alipenda umma wa Watanzania uelewe kuwa hadaiwi
NHC.
0 comments:
Post a Comment