ACT-Wazalendo waitisha mjadala wa Azimio la Arusha


Abraham Ntambara

CHAMA cha ACT- Wazalendo, kinatarajia kufanya mjadala wa kitaifa katika kuadhimisha miaka 50 ya Azimio la Arusha kutafakari mafanikio na mapungufu yake katika Tanzania ya leo.

Hayo yalibanishwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma Ado Shaibu aliyesema kuwa mkutano huo wa kidemokrasia utafanyika Machi 25 mwaka huu jijini Arusha.

“Mkutano huu wa kidemokrasia, utajadili nafasi ya siasa za kijamaa na za mlengo wa kushoto barani Afrika na duniani katika zama hizi za kukua kwa kasi kwa siasa za mlengo wa kulia,” alisema Shaibu.

Shaibu alisema katika maazimisho hayo, ACT kitatumia mkutano huo kutafakari dhana na msingi wa Azimio la Tabora linalohuisha Azimio la Arusha katika mazingira ya karne ya 21.

Aidha alieleza kuwa mbali na viongozi wa chama hicho mkutano huo utawaaleta pamoja wanasiasa wa vyama mbalimbali, wawakilishi wa Asasi za Kiraia, wanazuoni na wanaharakati kutoka ndani na nje ya nchi.

Alisema wamekwishatoa mialiko na kufanya mazungumzo na vyama vya Labour (Uingereza), Economic Freedom Fighters–EFF (Afrika ya Kusini), Die Linke (Ujermani), na Syriza (Ugiriki) ili viongozi wao washiriki na kutoa maada kwenye mjadala huo.

Aliongeza kwamba watawaalika pia waliokuwa wanachama wa Taasisi ya Ruvuma Development Association (RDA) pamoja na wananchi wengine wa kawaida walioishi wakati wa Azimio la Arusha na kushiriki katika kulitekeleza ili watoe uzoefu wao.

Kwa upande mwingine chama hicho kimemtaka Rais John Magufuli kuongoza nchi kwa kufuata Katiba na Sheria, Shaibu alisema ni haki ya kila mswananchi kupata wakili wakumtetea mahakamani.

Shaibu alieleza kuwa Katika siku ya maazimisho ya kilele cha siku ya sheria Rais alikaririwa akisema kwamba waharifu wakikamatwa na vyombo vya dora washitekiwe upesi huku akitaka pia wakili atakayejitokeza kumtetea aunganishwe katika kesi.

“Kwa nia njeama kabisa, kama chama cha siasa hatuwezi kukaa kimya tunao wajibu wa kumkumbusha kuwa nchi hii inaendeshwa kwa mujibu wa katiba na sheria,” alisema Shaibu.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo