Wanaojichukulia sheria mkononi waua watano


Moses Ng’wat, Kyela

MKUU wa Wilaya ya Kyela, Claudia Kitta, amewaagiza madiwani, watendaji wa kata, vijiji na viongozi wengine wenye dhamana katika maeneo yao kuhakikisha wanajihusisha kikamilifu kusimamia na kutoa elimu dhidi ya mauaji holela yanayotokea baada ya watu kujichulia sheria mkononi.

Kitta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya hiyo, amelazimika kutoa agizo hilo, baada ya takwimu za makosa ya kujichukulia sheria mkononi wilayani humo kuonyesha kuwa, katika kipindi cha miezi miwili watu watano wameuawa na wengine kujeruhiwa.

Akitoa salamu za Serikali katika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo, Kitta alisema matukio hayo hayakubaliki na yanapaswa kukomeshwa mara moja kwa viongozi wote waliopewa dhamana kuhubiri amani.

“Niombe madiwani katika maeneo yenu hakikisheni mnasimamia amani ili kuepusha watu kujichukulia sheria mkononi na kukatisha uhai au kujeruhi watu wengine wanaowatuhumu kuwa ni wakosefu kana kwamba wana haki ya kufanya hivyo,” alisisitiza Kitta.

Alisema ndani ya miezi miwili ya Desemba 2016 na Januari mwaka huu, takwimu zinaonyesha kuwa watu watano uhai wao umekatizwa kutokana na tabia ya watu kujichukulia sheria mkononi na wengine kadhaa kujeruhiwa.

“Hakuna mtu mwenye haki ya kutoa uhai wa mtu mwingine au kujeruhi  hata kama amekosa, watuhumi wanatakiwa kufukishwa kwenye vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake, hivyo elimisheni watu kuacha vitendo hivyo na watakaobaini hatua kali zitachukuliwa”.

Mkuu huyo wa Wilaya alisema ukiachilia mbali mauaji ya watu hao watano ndani ya miezi miwili, hivi karibuni mtu mmoja ambaye hata hivyo hakumtaja jina alijeruhiwa na kusababisha kung’olewa jicho baada ya wananchi kumshambulia katika vurugu zilizotokana na vijana wa kata ya Matema.

Kutaka kulazimisha kupewa ajira katika kampuni ya ujenzi ya kichina inayojenga barabara ya Kikusya hadi Matema, wakiutuhumu uongozi wa kampuni hiyo kufanya upendeleo kwa kuajiri vijana wengi kutoka nje ya Wilaya hiyo.

“Inasikitisha sana, Yule kijana nimeonana naye hivi sasa kapoteza jicho lake kwa sababu za watu kufanya mambo bila kujali sheria, hata kama wale wachina wamefanya hivyo, wananchi hawakupaswa kufanya kile walichofanya”.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo