Madereva bodaboda wahimizwa kutii agizo


Hussein Ndubikile

WAENDESHA bodaboda wa Dar es Salaam, wamesisitizwa kutekeleza agizo la Rais John Magufuli linalopiga marufuku bodaboda na bajaji kupita kwenye barabara ya mabasi yaendayo haraka (Udart) ili kuepuka usumbufu wa kupelekwa mahabusu na kutolewa matairi.

Hatua hiyo imekuja baada ya Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, kuanza kutekeleza agizo hilo kwa kukamata pikipiki 21 na kuzitoa matairi kisha kuwapeleka mahabusu madereva hao.

Akizungumza na gazeti hili jana, ofisa habari wa waendesha bodaboda hao, Abdallah Bakari alisema madereva hao wanapaswa kujua barabaara yanamopita mabasi ya mwendokasi hivyo hakitakiwi chombo kingine na kwamba dereva atakayekaidi atakumbwa na adhabu hiyo.

“Barabara ya mwendokasi inatumiwa na mabasi yake tu yanayoanzia Kimara hadi Feri, haitakiwiki bodaboda unashauriwa ukitaka kuvuka upande wa pili wa barabara ya mabasi hayo, tafuta sehemu yenye kivuko, shuka, sukuma pikipiki mpaka upande wa pili usipite eneo wanalopita waenda kwa miguu,” alisema.

Alisema bodaboda haitakiwi kuvuka eneo lisilo na alama ya kivuko huku akiwasihi kuacha kufanya biashara Feri na barabara ya Morogoro kwani kufanya hivyo ni kukaidi sheria za barabarani.

Alisisitiza kuwa kikosi hicho kimejipanga maeneo yote ambayo barabara hiyo imepita na atatoa ushirikiano kuhakikisha agizo la Rais Magufuli linatekelezwa.

Hivi karibuni, katika uzinduzi wa mradi huo, Rais Magufuli aliagiza kikosi hicho kukamata waendesha bodaboda na bajaj wanaokatisha kwenye barabara ya mwendokasi na kuwatolea matairi.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo