…Waliofanya vizuri walonga



Alfred

Mwanafunzi wa kwanza kitaifa, Alfred amesema siri ya ufaulu wake ni kusoma kwa bidii na kumtegemea Mungu huku akieleza kuwa alikuwa anatarajia kufaulu kutokana na jitihada alizokuwa nazo.

Alisema wakati akipigiwa simu kupewa taarifa hizo, alikuwa kwenye mafunzo ya udereva Mwenge alipoitwa kwa simu kutoka kwa Sekretari akamwambia mkufunzi wake amrudishe.

“Niliambiwa kuwa mama ananisubiri, nilipokwenda akaniambia nimeongoza matokeo ya kidato cha nne, sikuamini nililia kidogo lakini nikahisi kwamba mama ananitania, lakini ghafla akaniambia naitwa shuleni hivyo tukaanza safari,”alisema.

Alisema alipofika shuleni alishangaa wanafunzi wenzake wakiwa nje ambao walimwita huku na kule na kumpongeza lakini bado akawa hana imani hadi alipoitwa na vyombo vya habari kuhojiwa, ndipo akaamini kidogo.

“Yaani hadi sasa naona kama ndoto, sijaamini bado kama nimeongoza sina cha kusema zaidi ya kumshukuru Mungu na kuwasisitizia wanafunzi wengine kuhakikisha wanaishi katika ndoto ili waweze kuzitimiza,” alisema.

Mama

Mama wa Alfred, Adela Shauri ambaye ni mwalimu wa darasa la sita katika shule ya Msingi Mlimani alisema akiwa kazini alipigiwa simu na walimu wa shule aliyosoma Alfred, kumtaka aende shuleni hapo.

Alisema baada ya kuambiwa hivyo aliulizwa kuna nini, ndipo walipomweleza kuwa mwanawe ameongoza kitaifa kwenye matokeo hayo na kwamba baada ya kusikia hivyo alifurahi sana hali iliyochanganyika na kutetemeka.

“Ghafla nilitoka haraka nikaaga kwa Mwalimu Mkuu kwamba nimeitwa shuleni kwa Alfred nimepata dharura, hivyo nikachomoka nikaondoka kwenda kumfuata mwanangu chuo cha magari pale Mlimani,” alisema.

“Baada ya kumchukua Alfred nilimpigia baba yake ambaye anafanya kazi ya Uhandisi kwenye Halmashauri ya Bagamoyo akanieleza kuwa yuko kikaoni hivyo nimpigie baadaye lakini hadi muda huu hajui na hana taarifa, hivyo atakaponipigia nitamwambia,” alisema.

Akizungumzia siri ya ushindi wa mtoto wake, Mama Alfred alisema mwanafunzi huyo alikuwa anajisomea sana akitoka shuleni licha ya kuhudhuria vipindi na masomo ya ziada na alikuwa na ratiba zake binafsi.

Alisema Alfred alisoma shule za kawaida akiwa msingi na kwamba darasa la kwanza hadi la pilli alisoma shule ya JK Nyerere, Moshi, baadae Makongo hadi darasa la tano kisha shule ya msingi Mlimani.

Alisema shule ya sekondari alichaguliwa kwenda Ilboru, lakini wakampeleka shule ya wavulana ya Feza ambapo alipata punguzo la ada kwa asilimia 30 hali iliyosababisha unafuu kwa wazazi.

Mkurugenzi wa Feza, Ibrahim Yunus alisema Alfred amekuwa mwanafunzi bora katika masuala mengi na amekuwa mshindi wa kwanza kwenye uandishi wa insha na anatarajia kupewa tuzo mwezi huu.

Cynthia

Msichana wa pili kitaifa na aliyeshika nafasi ya kwanza kwa watahiniwa wa kike kitaifa, Cynthia Mchechu alisema ana ndoto ya kuwa mwanasheria.

Alisema ndoto ya kuwa mwanasheria aliianza mwaka 2009 wakati aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama ambaye aliapishwa mwaka huo akisoma baadhi ya vielelezo vyake kwenye mitandao ya kijamii.

“Ndoto yangu ya kuwa mwanasheria inamhusisha Obama kwa kuwa mwaka aliokuwa anaapishwa 2009 niliona vielelezo vyake vya uanasheria hivyo nataka kuwa kama yeye na naamini ndoto hiyo itatimia,” alisema.

Alisema wakati anapigiwa simu alikuwa ofisini shuleni kwao ambapo simu yake ilikuwa katika mlio wa kimya lakini mama yake akampigia simu ya mezani ili apewe taarifa.

“Kwa kweli nilipoambiwa siwezi kusema nilivyojisikia zaidi ya kulia kwa sikuamini kwa kuwa ni kitu ambacho kipo lakini bado sijaamini na sijakubali, lakini naamini haya yametokana na mimi kujisomea zaidi ya alichonifundisha mwalimu,” alisema.

Mama

Mercy Mchechu ambaye ni mama wa Cynthia alisema mtoto wake amekuwa akifanya vizuri siku zote na kwamba amekuwa mtu ambaye hufanya na husema vitu anavyoamini.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo