Jukwaa lataka taarifa Katiba Mpya


Leonce Zimbandu

Hebron Mwakagenda
JUKWAA la Katiba Tanzania (JUKATA) limetaka taarifa rasmi itolewe kwenye Gazeti la Serikali kwamba mchakato wa Katiba mpya uko hai na unaendelea ili kupata Katiba Mpya.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jukata, Hebron Mwakagenda, alitoa tamko hilo alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana.

Tamko hilo limekuja siku chache baada ya Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, kuzungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba na kuwaeleza kwamba Serikali itaanza kurekebisha sheria ili kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya.

Lakini Mwakagenda alisema kabla ya marekebisho ya sheria kuwasilishwa bungeni, itakuwa busara wadau kuyapitia ili kukubaliana eneo ambalo mchakato unapaswa kuanzia na kuepusha mpasuko wa kitaifa.

“Tunafahamu kuwa Profesa Kabudi ni nguli katika masuala ya sheria, hivyo atakuwa daraja la kufanikisha mchakato wa Katiba na hatimaye kupata mpya,” alisema.

Alisema tangu kuanzishwa kwa mchakato huo, wamepita mawaziri watatu na Profesa Kabudi atakuwa wa nne, alianza marehemu Celina Kombani, Mathias Chikawe na Dk Harrison Mwakyembe.

Alisema kutoka na weledi alionao Waziri, anapaswa kuwasilisha mswada wa marekebisho wa sheria ili kurekebisha sheria iliyosimamisha mchakato, huku Serikali ikijipanga kuipangia bajeti.

Mjumbe wa Bodi ya Jukata, Mpendwa Chihimba alipongeza hatua ya Profesa Kabudi ya kutaka Serikali ianze kufanya marekebisho ya sheria ili mchakato uanze.

Alisema hatua hiyo inapaswa kupongeza kwani haiwezekani Waziri azungumze na Kamati ya Bunge bila kuzungumza na kushauriana na Rais John Magufuli.

“Watanzania tuonde hofu, mchakato wa Katiba umo mbioni, hivyo hakuna sababu ya kukata tamaa,” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo